Kishore Kumar Hits

Ambwene Mwasongwe - Tulikotoka şarkı sözleri

Sanatçı: Ambwene Mwasongwe

albüm: Misuli Ya Imani


Tulikotoka ni mbali
Tukitazama nyuma
Asingekuwa Bwana
Tusingefika hapa
Yale tuliyoyapitia
Hayakutuacha tulivyo
Haikuwa rahisi
Ni mkono wa Bwana
Mengine yalikuja kama mema
Mwisho ukawa mbaya
Mengine yalikuja kama mabaya
Kumbe yanakusudi
Lakini katika yote hayo
Tulikuona Bwana
Ukitetea maisha yetu
Dhidi ya hatari mbaya
Tulikutana na hatari mbaya
Tukajua ni mwisho
Tulikutana na majanga mengi
Tukajua hakutakucha
Lakini katika yote hayo
Wewe ulisimama
Kutetea maisha yetu
Yasidhurumiwe
Yah Yah Yah ayayaya
Uuuuuuuh
Kaa nasi Bwana
Safari bado ndefu
Tunakumbuka mengi
Tuliyoyaona nyuma
Tunakumbuka mengi
Tuliyoyasikia
Tulipitia magumu
Yaliyotuchanganya sana
Tulipitia mengi
Yaliyotuvuruga mioyo
Tunakumbuka ndugu zetu
Tuliyowaacha nyuma huko
Tulitamani leo hii
Tungekuwa nao
Uuuuuuuh
Nakumbuka huyu alivyolia
Eehh eehh
Alipowakumbuka ndugu zake
Eehh eehh
Alitukaribisha kwao
Ayayaya
Akasema maneno haya
Jamani karibuni nyumbani
Hapa ndipo kwetu
Kwanzia huku hadi kule
Hizi ni nyumba zetu
Na kama mnavyoona
Wenyewe hawapo
Nyumba imebaki kimya
Na sisi tunaishi mbali
Ayayayaya aya
Mwingine alisimama
Akatafakari
Akapiga hesabu
Za maisha yake
Akaona mambo yake
Hayako sawa
Akatazama nyuma
Alikotoka akasema
Jamani niombeeni
Mambo ni magumu
Hali ninayopitia
Hata sielewi
Mwenzangu kabadilika
Siyo kama zamani
Hali inayoendelea
Sijui itakwisha lini
Ayayayaya
Ni kweli tunapita
Ni kweli yapo mengi
Yanayotusibu
Ila Mungu wetu
Yuko palepale
Ila wema wake Bwana
Uko pale pale
Katika yaleyale
Wengine wanayolia sana
Wapo wengine bado
Wanaimarisha
Katika yaleyale
Yanayowatoa roho wengine
Katika hayohayo wengine
Wanasonga mbele
Daudi anasema
Katika magumu yote
Nalimwona Bwana kasimama mbele yangu kumbe tatizo letu liko kwetu wenyewe tunaona magumu hatumuoni Bwana
Tatizo haliko kwa Mungu
Tatizo liko kwetu
Wala haliko kwa shetani
Tatizo liko kwetu
Tatizo ni sisi wenyewe vile tunavyoona
Hilo ndilo tatizo letu linalotusumbua
Songa mbele
Usitazame nyuma
Mtazame Bwana
Atakutia nguvu atakuinua na wewe usitazame nyuma mpendwa
Mtazame Bwana

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar