Kishore Kumar Hits

Ambwene Mwasongwe - Nguvu Ya Msamaha şarkı sözleri

Sanatçı: Ambwene Mwasongwe

albüm: Misuli Ya Imani


Alisikia minon'gono mtaani
Watu walikua wakiteta kuhusu yeye, masikini huyu hakujijua
Alijiondokea akitikisa kichwa chake
Asante sana Bwana umenisaidia, mabaya hayakunikuta mimi
Kumbe maneno yale yalikua yake, ila bahati mbaya hakuyajua
Alipoyasikia alidhani mapya, kumbe yalikua yanakwisha
Alipogundua yanamhusu, alihangaika ajitetee
Aliwalaumu sana rafiki zake kwa kujua, wamenyamaza
Jamani, jamani
Nyamaza, usilie...
Mungu atakusaidia, hajawahi kumtupa mtu
Nawe hatakutupa, nawe hatakutupa

Yakamshinda kuvumilia mabaya yale
Kila alipowaona wabaya wake, moyo wake ulipasuka
Akapanda gari asijue aendako, njia nzima alikua akiwaza
Kwanini Baba yangu, achukue mke wangu
Aliwalilia watoto wake, ninawaacha mkiwa wadogo
Sikutamani muishi hivyo, ila Mama yenu kasababisha
Ninakwenda nikafie mbali, ninasikitika hamtaniona
Nisameheni wanangu
Sitaki Babu yenu na Mama yenu, waone maiti yangu
Mwanangu (mwanangu) mwanangu sikia
Unadhani (unadhani) uchungu nilionao moyoni (nilionao)
Unaweza (unaweza) kuondoka kwa kuutoa uhai wako?
Unadhani utaridhika (kutoa) kutoa, uhai wako
Je, pia mwanangu (Je, pia) unadhani
Baya (baya-) ulilotendewa unaweza kufutika kwa kulipa kisasi
Kwa kulipa kisasi (kwa kulipa kisasi)

Malaika wa Bwana walimfuata, alikokwenda
Kila alipojaribu kujiua, mara zote hilo lilishindwa
Sauti ya Bwana ikasikika ikimwita, rudi nyumbani
Ukawaombe msamaha, Baba yako na Mke wako
Usiende kuwaambia watoto wako, ubaya wa Mama yao uliotendewa
Usije mlaumu Baba yako, mbele ya macho yao wakasikia
Mimi nakutuma nina kusudi, ukifika ukawaangukie
Nataka nijitukuze kwa nguvu ya msamaha, nenda nipo nawe
Usiogope (nyamaza)
Nyamaza (usilie) nyamaza, Mungu atakusaidia
(Hajawahi) hajawahi, tupa mtu (na hili nalo)
Nawe hatakutupa
Kwa hili nalo (nawe hatakutupa)
Unajua Mungu, unanionea
Wamenikosea, hawakuniomba msamaha
Nilipoondoka waliniona, japo Watoto wangu na Mama yangu sikuwaaga
Iweje leo unambie nirudi, nikawaombe wao msamaha tena
Wakati wenyewe walipaswa kuniomba msamaha
Ninajua moyo wako, ulivyoumizwa Mwanangu
Ndio maana nakutuma, upone
Ninakutuma nenda kawaonyeshe, nguvu ya msamaha ah

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar