Kishore Kumar Hits

Ambwene Mwasongwe - Ndoa şarkı sözleri

Sanatçı: Ambwene Mwasongwe

albüm: Misuli Ya Imani


Siku moja nilipigiwa simu
Ilikua simu ya mwaliko
Jumapili tutamshukuru Mungu kwa Sadaka ya pekee
Uje uimbe kanisani kwetu
Mda ulipofika wimbo ukaimbwa
Nao wakaja mbele
Wametanguliza kijana na binti mmoja
Msemaji wao akaanza kutoa hotuba fupi
Kabla sadaka haijatolewa
Mungu ninakushukuru sana Kwa.
Kwa kumponya binti yangu alieugua kichaa
Pia ninakushukuru kwasababu
Kijana huyu alionesha upendo wa ajabu
Nilipomwambia achana na mwanangu hakufai tena
Yeye alijibu nimempenda ntaoa ivo ivo
Sijawahi ona upendo kama huu
Sijawahi ona upendo kama huu
Upendo.
Upendo haupo katika maneno
Unaonekana kwa matendo
Hauonekani kwenye raha
Wathibitika wakati wa shida
Daima upendo una sura mbili
Japo wengi wanaijua moja
Wakati wa raha, faraja na nyimbo na zawadi kede kede
Wanaridhika na upendo huo
Ila upendo una kipimo chake wakati
Wa shida na raha na wakati wa magonjwa
Wakati ambapo waona tabia kasoro na mapungufu hapo ndipo upendo upimwa
Yule anaeweza kusimama na wewe wakati wengine kawaida wangekukimbia
Tena awezae kukufichia aibu wakati wengine ni kawaida wangekutangaza
Yule ambae hapendi kuona unaharibikiwa
Hata mkikosana hapendi kuona unateseka
Huyo ndie mwenye upendo wa kweli
Huyo ndie mwenye upendo wa kweli
Upendo upendo Upendo
Haupo katika maneno, unaonekana kwa matendo
Hauonekani kwenye raha huthibitika.
Wathibitika wakati washida, wathibitika.
Wathibitika wakati wa shida
Watu Duniani wanaangaika
Kupenda vinavyopendeza
Wanasahau kupenda vinavyopendeza
Hakuna thamani, isipokua kupenda visivyo pendeka
Kama mkiwapenda wale wawapendao
Mwafanya ziada gani wapendeni waombeeni wanaowaudhi
Baba yenu wa mbinguni atawapa thawabu na watu watasema huu ndio upendo wakweli
Jipime kama kweli wewe unaoupendo Ulifanyaje
Nduguyako alipokukosea
Ulimsengenya au ulimuombea
Ulimpenda bure au ulimpaka matope
Ulimsengenya au ulimuombea
Ulimpenda bure au ulimpaka matope
Jijibu kama una upendo wa kweli
Jijibu kama una upendo wa kweli
Upendooo.
Upendo haupo katika maneno unaonekana kwa matendo
Hauonekani kwenye raha
Huthibitika wakati wa shida
Wathibitika wakati wa shida
Upendo haupo katika maneno
Unaonekana kwa matendo
Hauonekani kwenye raha
Wathibitika wakati wa shida
Wathibitika wakati wa shida
Kanisa lote lilinyamaza
Binti akapewa nafasi aseme
Akalia sana... Akishangaa
Sijawahi ona upendo kama huu
Sijawahi ona upendo kama huu
Akalia sana mbele za Mungu, akanyoosha mkono atoe sadaka
Najua uliniponya sikwaajili yangu
Ukutaka aaibike na upendo wake
Ukutaka aaibike na upendo wake

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar