Kishore Kumar Hits

Ambwene Mwasongwe - Natamani şarkı sözleri

Sanatçı: Ambwene Mwasongwe

albüm: Misuli Ya Imani


Natamani sana,
Niwe kama bwana,
Mtu mwema sana,
Alie jikana,
Niwe mpole,
Niache ya kale,
Nitazame mbele,
Daima milele,
Niwe mtiifu,
Tena mwaminifu,
Mtakatifu,
Asiyejisifu,
Mnyenyekevu na mvumilivu,
Mtu mtulivu, asiye na wivu.
Bwana ulikuja, Duniani hapa,
Kuleta ukombozi kwa kila kilichopotea,
Ulianza na mimi niliyedhaifu,
Ukaniinua kutoka matopeni,
Wewe ulikuja kuleta suluhu ya makosa yote mwanadamu aliyokosea,
Ulikuja kutibu kosa la mwanaume,
Alilolifanya bustani ya edeni,
Mwanaume akikosea Dunia yote huyumba,
Mwanaume akikosea watu hujutaa,
Kila jambo ulionalo linayumba Duniani limetokana na makosa ya mwanaume,
Leo natamani hii yaani,
Niweze kuwa kama wewe bwana,
Niweze kushinda yote magumu,
Ya ya yaani.
Natamani sana,
Niwe kama bwana,
Mtu mwema sana,
Alie jikana,
Niwe mpole,
Niache ya kale,
Nitazame mbele,
Daima milele,
Niwe mtiifu,
Tena mwaminifu,
Mtakatifu,
Asiyejisifu,
Mnyenyekevu na mvumilivu,
Mtu mtulivu,
Asiye na wivu.
Nimevutiwa na historia yako,
Wewe bwana wangu Yesu ni wa ajabu,
Kabla ulimwengu haujakuwako,
Ulikuweko miaka mingi ya nyuma,
Umeishi na wapole,
Umeishi na watakatifu,
Umeishi na wenyenyekevu kama Enoko,
Umeishi na watu wa kila aina,
Wenye maombi na upako kama Mussa,
Pia umewahi kutana na magaidi,
Kama Farao na watu wenye roho ngumu,
Una uzoefu wa kuishi na watu,
Wenye tabia ngumu,
Hiyo ndio sifa yako,
Naamini leo ukiwa ndani yangu bwana,
Nitaweza kushinda maisha yoteee,
Kaa kwangu uniongoze mimi natamani sana kuwa kama wewe.
Niwezeshe wewe bwana wangu oooh,
Nataka kushindaa yoote,
Ya ya ya.
Natamani sana,
Niwe kama bwana,
Mtu mwema sana,
Alie jikana,
Niwe mpole,
Niache ya kale,
Nitazame mbele,
Daima milele,
Niwe mtiifu,
Tena mwaminifu,
Mtakatifu,
Asiyejisifu,
Mnyenyekevu na mvumilivu,
Mtu mtulivu,
Asiye na wivu.
Nataka kufuata nyayo zako,
Nataka kufuata hatua zako,
Nataka kufuata upendo wako,
Ulioacha enzi kuja kwetu hapa,
Ulimpenda mwanadamu asiye na sifa,
Ulimpenda mwanadamu asiye na vigezo,
Ni upendo tu uliokugharimu maisha,
Umkumboe yeye ili apate upako.

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar