Kishore Kumar Hits

Ambwene Mwasongwe - Ombi langu şarkı sözleri

Sanatçı: Ambwene Mwasongwe

albüm: Ombi Langu


Mmh, Haleluya
Huuapia moyo
Ntakulinda maana najua kwamba
Kuna chemichemi
Ntakujengea boma uwe salama
Adui akija asikuweze
Usiruhusu maneno yakuvuruge
Usiruhusu hasira ikae kwako
Ntamuweka mlinzi awe ngome yako
Akupiganie ubaki salama
Bwana naomba utete nao wale
Wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sistaili kubishana nao
Sitaki kupambana nao nisije nikakosea Wakanilaumu
Maana wameshavuta upinde wapo kwenye
Mangojeo yao wamenuna wamekunja sura Wanahasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru ni kwamba Hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee waninase
Usiache mguu usogezwe unase kwenye mitego Yao
Weka mgojenzi, kinywani mwangu
Anilinde nisiropoke
Heeeeeee hili ni ombi langu kwako Mungu Akukumbuke na wewe
Katembee na wewe hata uwapo gizani akulinde
Wewe ni wimbo wangu tena dawa ya moyoni Mwangu
U fahari yangu
Haaa haaaa haaaa haaa
Nifanye kama Yusufu uliemuona muota ndoto Ukam-bariki
Wewe ulimuona waziri mkuu tofauti na Wanadamu
Wakamtazama vingine walivyoweza
Baba yake alimuona mpelelezi awapeleleze Ndugu zake
Ndugu zake walimwona ni mmbea wakamtupa Shimoni
Wamediani wakamwona biashara wakamuuza Kwa Potifa
Mkewe Potifa kamtamani akamuona kijana Mzuri
Wafungwa wenzake wakamsahau wakifikiri ni Mhalifu
Wewe uliona ndoto ndani yake ukamfanya Waziri mkuu
Nami nifanye kama Yusufu
Hili ni ombi langu kwako Mungu akukumbuke Na wewe
Katembee na wewe hata uwapo gizani akulinde
Wewe ni wimbo wangu tena dawa ya moyoni Mwangu
U fahari yangu hata...
Wewe ni kisima kwako nitachota hekima, kwako Nitachota baraka
Kwako nitachota wema
Kwako nitachota ukuu
Kwakooooh
Kwako nitajifunza
Kwako nitaburudika

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar