Kishore Kumar Hits

PAUL CLEMENT - WAGENI şarkı sözleri

Sanatçı: PAUL CLEMENT

albüm: SERMON


Katika maisha yangu
Nilipokea wageni
Nikawakaribisha kwangu
Wakafanya vitu vingi
Hawakuwa wa kudumu
Walikuwa wapitaji
Ila moyo wa ukarimu
Ukanisababishia machozi
Mgeni wa kwanza alikuwa ni uchungu
Akaniumiza, akanipa maumivu
Alipomaliza akaenda zake
Mgeni wa pili alikuwa ni huzuni
Huyu naye
Akanikosesha furaha
Mgeni wa tatu alikuwa ni magonjwa
Akanidhoofisha, akataka kuniua
Hakufanikiwa akaenda zake
Aliyefuata alininyima watoto
Jina lake tasa
Naye alipita
Mgeni mmoja jina lake ni mauti
Akamchukua Ntimi, akaniachia jeraha
Mgeni mwingine jina lake hofu
Hakutaka nifanikiwe
Akanipa fikra potofu
Nikajiona siwezi
Tena nitafeli
Huyo naye alipita
Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Hawa ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Hakuna jambo lolote gumu
Litakalodumu kwenye maisha yako
Ila yote yatapita
Na yakishapita
Hayatarudi tena
Tough times never last
But tough people do
Mapito siyo mambo magumu unayoyapitia kwenye maisha yako
Ila mapito ni mambo magumu yanayopita kwenye maisha yako
Ndiyo maana ninaita mapito, kwa kuwa yanapita tu
Na yanapita kwenye maisha yako,
Na yakishapita hayawezi kurudi tena, ah
Magonjwa,
Hao ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Uchungu, (Huzuni)
Hao ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Mateso, (Changamoto)
Hao ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
(Hata dhiki)
Hao ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar