Waambie mbie Usingizi kanitoroka, Moyoni nimekesha ngoma Kwa subira nimengoja, penzi hili la thamana Tangu tulipokutana, nafsi zetu kapatana Na ni mbali tumetoka tangu kuchumbiana Siku yetu imefika hakuna atayezuia Ajaliye Maulana, pete tutavishana Waambie mbie Nimeshapatikana na yule mume Wa mapenzi shanienzi Waambi mbie Milele nishazama Sinitafute kule kwa mabinti nishahama Angalia ishara Tazama ishara Mi nishahama Angalia ishara Tazama ishara Mi nishazama ♪ Kuna wale wanasema ndoa haidumu tena Yaje maji na mafuriko tayari tushatiya nanga Nimepata yule wangu kampenda na vyote vyangu Sitaja sahau amenivisha dhahabu Nimepata yule wangu kampenda na vyote vyangu Simulie walimwengu nishampaa moyo wangu Waambie mbie Nimeshapatikana na yule mume Wa mapenzi shanienzi Waambie mbie Milele nishazama Sinitafute kule kwa mabinti nishahama Angalia ishara tazama ishara Angalia ishara mi nishahama Angalia ishara tazama ishara Angalia ishara mi nishazama Ee Mola tusaidie kwa wema wako Tuwe na ndoa yenye furaha Milele hadi milele Waambie mbie Nimeshapatikana na yule mume Wa Mapenzi shanienzi Waambie mbie Milele nishazama Sinitafute kule Kwa mabinti nishama