Kishore Kumar Hits

Goodluck Gozbert - Huwezi Kushindana şarkı sözleri

Sanatçı: Goodluck Gozbert

albüm: Huwezi Kushindana


Hauwezi kushindana, oh kushindana
Na mwanadamu mwenye kinywa
Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu
Mbona sasa ningekuwa na vidonda mwili mzima
Vita vya maneno kuna watu ni majemedari
Ukisema mshindane mbona mikono mtainua
Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue
Wewe ni mti wenye matunda zoea mawe
Lia kidogo nyamaza ili uchungu uishe
Ukiendelea unawapa kichwa hao
Basi laza imani rejea vitani
Wakikuona waseme umekuwa sugu
Acha waongee acha waseme seme
Ila yuko Mungu wakuwaziba midomo
Ikiwa Mungu anahukumu kwa kusikiza maneno
Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana
Hivi Mungu angehukumu kwa kusikiza umbea
Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa
Mwanadamu mwanadamu shida ni ulimi
Ungejifunza ukimya haunanga hasara
Fulani we fulani una shida gani
Na uongo wanini Mwogope Mungu
Ukumbuke ni ahadi kuna siku yaja
Kwa kila neno na kinywa chako utatolea hesabu
Mimi nimeshakwambia

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar