Kishore Kumar Hits

Remmy Ongala - Muziki Asili Yake Wapi şarkı sözleri

Sanatçı: Remmy Ongala

albüm: Songs for the Poor Man


Muziki asili yake wapi eeeee
Muziki ni wa nani eeeee
Muziki hakuna mwenyewe
Muziki ni mwito
Muziki ni fundisho
Muziki maombolezo kilio
Usinione nikiimba
Ukadhani ninayo furaha
Kumbe ninayo huzuni moyoni
Muziki alivyo na nguvu ulimwenguni kote
Hata makanisani wanaimba kwaya kwa kumuomba Mungu
Kumuabudu Mungu
Kwa kumsifu Mungu
Hata kukiwa sherehe za serikali,mbele ya Mwenyekiti kuhutubia
Ni Muziki unaanza kuwakusanya watu
Kumbuka Paulo na Sila waliimba gerezani Mungu amewasikia
Kumbuka Musa aliimba Muziki wa aina yake
Kuwakomboa wana wa Israeli
Waliopo utumwani katika nchi ya Misri
Kukiwa na sherehe utaimba nyimbo za furaha
Kukiwa na tabu utaimba nyimbo za masikitiko
Ukifa leo utapelekwa kaburini na nyimbo za maombolezo
Ni muziki pekee ulio na nguvu
Utawakusanya wabaya na wazuri msiku ya mwisho Mungu akitoa hukumu
Muziki sio uhuni
Kama muziki ni uhuni kwa nini unanunua kaseti
Kama muziki ni uhuni kwa nini unaomba nyimbo redioni
Kama muziki ni uhuni kwa nini kwa nini unanunua rekodi
Kama muziki ni uhuni kwa nini unacheza muziki weeee
Kama muziki ni uhuni kwa nini unafanya top ten show
Kumbuka siku ya mwisho ikifika
Kutakuwa mlio mmoja wa parapanda utawakusanya wateule wote
Walioteuliwa katika pembe nne za dunia
Siku ya mwisho Mungu akitoa hukumu,hukumu,hukumu
Hata kwa Mungu malaika wanaimba ooh
Muziki asili yake wapi eeeee
Muziki ni wa nani eeeee
Muziki hakuna mwenyewe
Muziki ni mwito
Muziki ni fundisho
Muziki maombolezo kilio
Usinione nikiimba
Ukadhani ninayo furaha
Kumbe ninayo huzuni moyoni
Muziki asili yake wapi eeeee
Muziki ni wa nani eeeee
Muziki hakuna mwenyewe
Muziki ni mwito
Muziki ni fundisho
Muziki maombolezo kilio
Usinione nikiimba
Ukadhani ninayo furaha
Kumbe ninayo huzuni moyoni

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar