Kishore Kumar Hits

Siti Muharam - Nyuki şarkı sözleri

Sanatçı: Siti Muharam

albüm: Siti of Unguja (Romance Revolution on Zanzibar)


Nyuki wanisikitishah, Ukweli nakuelezaah
Asali unozalisha viumbe yatupendezaah
Kumbe waitaarisha kwa vitu vilivyo oza
Ungelinifahamisha, Ungelinifahamisha
Ungelinifahamisha, kuila nisingeweza
Nawauliza mashekh pamoja na wanazuoni
Asali khalali yake naomba njulisheni
Asijeipiga teke, Asijeipiga teke, Asijeipigateke, akaitoa thamani
Nyuki waenda porini mizoga kuitundua
Hata mzoga wa nyani nyuki wajichukulia
Waja na chumo kinywani, asali kutengezea
Ukiiona dukani, Ukiiona dukani,
Ukiina dukani, viumbe twaigombea
Viko vingi duniani vikioza ni haramu
Navitoke ugenini nchini viwe adimu
Ukila uhatiani watu watakushutumu
Hii asali kwanini, Hii asali kwanini,
Hii asali kwanini, i khalali kila awali
Utamu wake asali hakika umezidia
Nitamu kushinda wali au nyama ya ngamia
Kaitunuku Jalali khalali kuitumia
Ukiila kwa kikiri, Ukiila kwa kikiri,
Ukiila kwa kikiri, unaweza ukasinzia

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar