Eeh Mungu Nguvu Yetu, Ilete baraka kwetu, Haki iwe ngao na mlinzi, Natukae kwa Undugu Amani na Uhuru, Raha tupate na ustawi. Amkeni Ndugu zetu, Tufanye sote bidii, Nasi tujitoe kwa nguvu, Nchi yetu ya Kenya, Tunayoipenda, Tuwe tayari kuilinda. Natujenge taifa letu, Ee ndio wajibu wetu, Kenya istahili heshima, Tuungane Mikono, Pamoja Kazini, Kila siku tuwe na shukrani.