Kishore Kumar Hits

Zabron Singers - Naogopa şarkı sözleri

Sanatçı: Zabron Singers

albüm: Niko Sawa


Naogopa nikiwaambia watu sijui wataniona vipi
Naogopa kuyasema yote acha tu ninyamaze kimya
Naogopa kuwaambia watu wanaanza kunisengenya
Nina maswali mengi, miguuni Pako
Kwa nini Mungu, umekuwa kama vile huoni?
Pesa sina, lakini umeacha niugue
Namtegemea lakini umemwacha aondoke
Kwa nini Mungu umenyamaza?
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali
Umenyamaza
Maumivu ni makali na vita ni vikali
Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali
Umenyamaza
Maumivu ni makali na vita ni vikali
Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu
Mbona kwa yule Ulitenda juzi, na leo tena
Una ugumu gani kwangu Baba, sema basi
Mimi binadamu nakosa majibu, sema Baba
Nakuamini sana Baba yangu, Usiniache
Kuna shida gani, imekuwaje? Hata Usiseme
Kama ni kosa naomba Unisamehe
Urekebishe naomba Unisamehe
Nateta Nawe sitokata tamaa
Wa kuamua yangu bado ni We
Nakuamini Mungu bado ni We
Naogopa uko kimya kuna nini Mungu?
Sema neno Usikae kimya
Mi'sijakufuru Mungu
Kama siku zangu za kuishi duniani bado zipo
Naomba sasa Baba Umalize, Umalizane na shida zangu
Mambo mengi nimeomba Kwako
Umejibu, hili hujajibu
Mungu wangu, bado nasubiri Kwako
Jibu basi, watu wakuone Wewe
Watu wakuone Baba
Bado nasubiri Kwako
Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali
Umenyamaza
Maumivu ni makali na vita ni vikali
Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu
Maumivu ni makali na vita ni vikali
Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar