Zikufikie salama mama mzazi, Mama uliyenizaa si anti si shangazi, ulimwengu umeniadaa, Siwezi kukataa, Siwezi kushangaa, Nashika adabu japo siwezi kufa njaa, yamenikuta sasa najuta nafanya ibada, , Dunia darasa leo nasoma bila ada, , Soma jarada nimebambikiwa mada, , Nimepakaziwa nimeshitakiwa mara saba, Msalaba huu, Nimeubeba bila hatia, Nilimwambia jaji na hakutaka kunisikia, Kanizawadia maisha yenye gundu na kiza, Kasahau kwamba hatuendi kwa mungu kwa viza, Sikiliza mama sikiliza maana inaniumiza sana, Ili nifungwe jela ndo wakafanyiza njama, Si trela si drama ulitazama halisi, Kwenye kizimba cha mahakama pata maana dadisi, Na ni rahisi kua hapa although how i play that nice, Polisi ndo wametaka never blame that life, Wako toka jela mwanao pokea salam mahututi kwenye machela huku maisha sio matam.