Nilikutana nae pande za Kinondoni Mida ya saba mchana ilisema saa ya mkononi Stendi ya daladala maarufu kama Morocco Mi natokea Mbagala naenda pande za King'oko Ghafla, nikashtuka alivyonigusa bega Kwa gadhabu milipogeuka ni yeye nikaona shega (Ila) sikuamini nilipomuona, kwamba ni bibi Au msichana mdomo kushona, ikanibidi Namkumbuka nilisoma nae shule ya msingi Ndugu hawana mpango nae tangu alipokufa dingi Darasa la saba nauhakika hakumaliza Usawa ulikaba akikumbuka inamuumiza Yamemsibu rafiki ukimuona huwezi kumjua Kachakaa hatamaniki hana viatu anapekua Dhambi kumpa kisogo hana tiba anapougua Shida zake tangu mdogo sasa mtu mzima amekua Siku ikipita hajala inshaallah, Mola anajua Wapi usiku atalala ni msala, anaomba dua Anatamani kufa msalaba apate kuutua Kafeli kujiua, Mungu hajapenda kumchukua [Chorus – I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high [Verse 2 – Kumbe alipata kazi ya usafi ndani ya kanisa Na nyumba ya mwiinjilisti aliamini nyoka wa Kibisa Maisha yakaendelea, mara zikaanza visa Alipoguswa akalegea, pasta nyavu akatikisa Lisa aka-surrender kama mtuhumiwa kortini Akasahau kalenda kwa utamu wa penzi ofisini Kila starehe alitenda zaidi ya pasta na muumini Mwazimu aligeuka mwenda aliyempenda kiongozi wa dini Alimchengua akili na kumuondolea usichana Mengine akaona sio dili, ngono ndo tamu sana Kakesha akisubiri, maana anajulikana Miezi ni kumi na mbili ila hata mmoja hakuonekana Akamfungia safari, pasta aliyempenda jana Bahati mbaya hakuwa tayari kuikubali akamkana Mbele ya umati akamuumbua sio yake wakaachana Akamuapia angemuua endapo kwake angeonekana Akaipoteza imani, akazamia mitaani Kwa ushetani wa pasta feki ambae hivi sasa yupo ibadani Maisha yake hayaendi poa Aliyemtamani amemtapeli Mimba alifaulu kuitoa Ila ukimwi amefeli [Chorus – I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high [Verse 3 – Kizuri daima hakidumu Shida kitaletewa Suluhu sio kunywa sumu Wherever anaenielewa Ye nini maisha magumu, kila kitu amepewa Ukimwi hatoulaumu kwa biashara ya mwili Sewa Masikini na vibopa ye anawapa mdudu wa karne Kama hauna leo unakopa, ye kwake mteja ni mfalme Panda usiku, panda mchana ukihitaji mwezini sana Jeneza hofu urefu, nishaukadiria upana Wa msichana Vidume vinapangwa toka Ukonga hadi ubungo Msichana anatwangwa na kupetwa kama ungo Msiogope kuzichanga anauza bei nafuu Kashayavuka tai ya Langa, matawi ya juu Kashaipoteza dira, life gumu aliopitia linamtia hasira Future amemaliza, malengo hayajajatimilika Kifo amebakiza, najiuliza kesho itafika ni patashika [Chorus – Grace Matata] x3 I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high I'm sitting in my room Thinking back on you, memories high