Kishore Kumar Hits

Ambassadors Of Christ Choir - Tugire Urukundo şarkı sözleri

Sanatçı: Ambassadors Of Christ Choir

albüm: Tugire Urukundo


Je umekumbuka kumuombea yule umpendae,
Jamani twazingira na maovu mengi kwahyo yatupasa kuombeana sana
Mtoto wako atoka asubuhi sana kwenda shule,
Sokoni na kadhalika apitapo kumejaa
Mabaya mengi sana mama mwombee mtoto wako
Apitapo ajali ni nyingi (mwombee mtoto wako)
Mbwa wakali wamzingira(mwombee mtoto wako)
Siku hizi vibaka ni wengi (mwombee mtoto wako)
Oooooh ooh (mwombee mtoto wako)
Ewe mama watenganishwa na Mme wako kaenda safari ya mbali kikazi,
Je umemwombea kule aliko mbali na
Wewe kumbuka amezingirwa na maovu mengi
Kule nasikia kuna wachawi(mwombee Mme wako)
Na wenzake kumwonea wivu(mwombee Mme wako)
Kuelewana na mabosi zake (mwombee Mme wako)
Afya njema asiugue(mwombee Mme wako)
Ewe baba watenganishwa na mke wako kaenda safari ya mbali shuleni je
Umemwombea kule aliko mbali na
Wewe kumbuka amezingirwa na maovu mengi
Kamwombee sana mke wako (mwombee mke wako)
Aweze kufaulu shuleni (mwombee mke wako)
Majaribu mengi yampata(mwombee mke wako)
Uvumilivu kwa kila jambo(mwombee mke wako)
Ooh oh oh (mwombee mtoto wako)
Ooh oh oh(mwombee Mme wako)
Ooh oh oh(mwombee mke wako)

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar