La Familia Chid Benz Aaaa Ali Kiba Hasira za nini kwanini huniamini Kama mwenzio nakupenda Maneno mengi mjini ili uniache mimi Lakini mwenzio bado nakupenda ×2 Chakula hakiliki kama nisipo kuona Haipiti chai, iriki wala ndafu iliyo nona Lazizi waubani (chumba) mashallah Mola kweli aliumba Huna kasoro umejazika mlaini kama godoro kiuno unakatika Nabangaiza vibarua mchana usiku japo nipate chochote nije tule ipite siku Maneno ya waongo waharibu makusudi usafiri mjini wa taabu ninapo chelewa kurudi usinihisi vibaya ukanuna, ukavimba ukatamani unirarue ugeuke simba (Ugeuke simba baby hasira za nini) Hasira za nini baby Hasira za nini kwanini huniamini kama mimi mwenzio bado nakupenda maneno mengi mjini ili uniache mimi lakini mimi mwenzio bado nakupenda ×2 Mamy punguza hasira na unisikilize mimi please acha kuzira hivyo nami hunithamini Sina mwingine zaidi yako haki ya nani moyo wangu upo kwako kwingine sito tamani Nilizunguka pande zote nikaona warembo wote Kote nilisimama kwako naanguka niokote Unanipa morali ya kutafuta mapesa najaza kibubu maisha mbele yasije kututesa Pesa ndio kila kitu nazisaka mchana usiku Sipendi sipendi kuishi kwa karaha nakwambia kila siku Popote kambi chochote pwani ndio life honey Sitaki tuje lia njaa nazisaka nje ndani Jasho langu ili upate isikukumbe tamaa Japo nilite mkate wakinishinda dagaa Nipende usiniache mamy usije tambaa Napo kukumbata nikumbate wangu wa shida na raha Hasira za nini mamaaa La Familia Chid benz hapa Hasira za nini kwanini huniamini kama mimi mwenzio bado nakupenda maneno mengi mjini ili uniache mimi lakini mwenzio bado nakupendaa ×2 Usinihukumu vibaya kwa maneno ya watu wabaya wasiopenda maendeleo kwa watu ×4