Kishore Kumar Hits

UPENDO NKONE - Yesu Naja Kwako şarkı sözleri

Sanatçı: UPENDO NKONE

albüm: Uniongoze Yesu, Vol.4


Nimefanya uchunguzi
Nimegundua Yesu ni mwamba
Msaada wa karibu
Tena nguvu ya wenye haki
Ana upendo na watu wake
Baraka zote ziko kwake
Niende wapi niyapate mema
Siitaki kwenda kwa mwingine
Yesu wangu
Mimi nakuja kwako
Wengine wamekua ni wezi
Na wengine ni makahaba
Wako pia majambazi
Eh Mungu waokoe
Sitaki kufanya maovu hayo
Baba yangu nimeona
Nije kwako
Nihurumie mwamba
Wako waendao kuzimu
Ili kupata mafanikio
Watumishi wengine nao wategemea nguvu za mapepo
Siutaki msaada wa mapepo
Yesu wangu nautaka msaada wako
Uniwezeshe Yesu
Hata kama utakawia
Nitazidi kuvumilia
Ninayo imani moyoni
Siku moja utanikumbuka
Hee. kwa nini nitende dhambi kubwa
Namna hii nikukosee
Mungu wangu
Uniepushe Baba yangu

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar