Kishore Kumar Hits

Reuben Kigame - Hapana Jina Jingine şarkı sözleri

Sanatçı: Reuben Kigame

albüm: Wastahili Bwana


Sijui unaposikiliza hizi nyimbo unawaza nini
Pengine wapitia katika shida mbali mbali
Na dunia na magumu yake yamekukumba
Pengine moyo wako mzito
Washangaa, kimbilio utalipata wapi?
Nina ujumbe mwema kwako
Kuna mmoja ambaye akupenda
Na unaweza kumtolea maisha yako yote
Naye atakuweka salama
Yeye ni Bwana, Yeye ni Mungu
Zaburi ishirini na tatu ya tuambia
Bwana ndiye mchungaji wangu
Sita pungikiwa na kitu
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza
Kando ya maji ya utilivu huniongoza
Hunihuwisha nafsi yangu
Nakuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake
Naam, nijapo pita kati ya bonde la uvuli wa mauti
Sitaogopa mabaya
Kwa maana wewe upamoja nami
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji
Waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu
Umenipaka mafuta kichwani pangu
Na kikombe changu kinafunika
Hakika wema na fazili zitanifuata
Siku zote za maisha yangu
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana, milele

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar