Kishore Kumar Hits

Reuben Kigame - Enda Nasi şarkı sözleri

Sanatçı: Reuben Kigame

albüm: Ombi Langu


Hufika wakati katika maisha ya binadamu ambapo tunafanya mambo bila ya Mungu kuwa nasi
Ni vema kufahamu kwamba asipoenda nasi, haitawezekana sisi kufaulu
Kama Musa nawa Israeli, tuombe Bwana tafadhali, enda nasi
Hili liwe ni ombi lako siku ya leo

Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe bwana wa majeshi tusikie
Kama huendi nasi, hatutaki kutoka hapa
Hatuwezi peke yetu, enda nasi
Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako turehemu (tusafishe)
Tusafishe e baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako, enda nasi (mm-hm)
Tutavua, mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu (mioyo yetu)
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi
Tunaomba utuonyeshe njia zako (kwa maana)
Kwa maana umetuita kwa jina lako
Twalilia e bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa, enda nasi
Oh, Bwana
Tutavua, mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi
Ndugu na dada yangu, tafadhali
Usijaribu kuyamudu maisha bila yake Bwana, utashindwa
Yafaa tufike mahali ambapo Musa alimlilia bwana na kutafuta uso wake
Na kusema, "Bwana tafadhali, enda nami, enda nasi, twakuhitaji" whoa
Tutavua (tutavua), mapambo yetu (mapambo yetu)
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako (twaleta Baba)
Tutakase na utembee nasi (tutavua)
Tutavua, mapambo yetu
Vitu vyote vya dhamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi (mioyo yetu)
Mioyo yetu twaleta mbele zako (tuna leta mbele zako)
Tutakase na utembee nasi
Oh, Bwana, tembea nasi
Bila wewe tutashindwa
Hili ni ombi letu, Baba

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar