Kishore Kumar Hits

Reuben Kigame - Njoo Sasa şarkı sözleri

Sanatçı: Reuben Kigame

albüm: Usifadhaike


Nilikuumba unitukuze, uyafanye mapenzi yangu
Kabla kuzaliwa na mama yako, nilikujua na kukupangia
Mambo mema maishani, kwa kuwa mimi ni mungu wako
Kwanini wanitoroka, kana kwamba nimekukosea?
Ae, ae, fungua macho, ona maisha yalivyo mafupi
Ae, ae, ukifa sasa, utaacha faida gani?

Elimu mimi nimekupatia, ukaitunia kunikashifu
Pesa na mali nikakupa, ukavitumia kunidharau
Sura nzuri nilikupa, ukaitumia kwa kujiuza
Mbona sasa wahangaika? Maisha yako yameporomoka
Ae, ae, ninakuomba, unirudie nikusafishe
Ae, ae, ninakupenda, mimi mungu wako ni wa rehema

Roho yako (eh, naitaka sasa)
Niitakase (eh, naitaka sasa)
Akili yako (eh, naitaka sasa)
Dhamira yako (eh, naitaka sasa)
Niitumie (eh, naitaka sasa)
Unitukuze (eh, naitaka sasa)
Siku zote (eh, naitaka sasa)
Mwili wako (eh, nautaka sasa)
Niutakaze (eh, nautaka sasa)
Njoo leo (eh, nakutaka sasa)
Nikuokoe (eh, njoo sasa, ah)
Umeumia, eh, njoo sasa, ah
Uta pona (eh, njoo sasa, ah)
Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Nikaribiye (eh, njoo sasa, ah)
Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Hujachelewa (eh, njoo sasa, ah)

Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Nikaribiye (eh, njoo sasa, ah)
Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Hujachelewa (eh, njoo sasa, ah
Nikutakase (eh, njoo sasa, ah)
Nikaribie (eh, njoo sasa, ah)
Njoo sasa, ah (eh, njoo sasa, ah)
Tusemezane (eh, njoo sasa, ah)

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar