Kesho nafasi ya kuanza upya Kumaliza kuishi nafasi ya kuanza kufa Kuivunja sheria nafasi ya kufuata ruksa Kuikumbuka jana au kuanza kuifuata future Future ni leo siku ambayo miti hukimbia Jua hushuka upendo, marafiki hufifia, [hufifia Wimbi la wanafiki huingia Kesho ya tumaini hubakia Tumaini, shika walau shika walau Na ujifunze kuziba kombe pindi anapopita nyang'au Akishapita tenda wema halafu kisha sahau Na uchunge unaponena watakuzika wadau Wadau, walikua uchi ukawavika mavazi Nyumba yako ikavunjika wakakunyima hifadhi Je, utasamehe utasahau kulipa kisasi Au kesho itakukuta umeshika risasi Risasi inawaza wapi itakukutia kesho Utatoroka kambi ama utavungia ghetto Tusipofikia lengo, utahama ukoo kwa kitu kidogo au utaitumikia nembo Nembo ya mjeshi ninayekaza mwendo kishujaa Kama unavyokaza nyonga kwenye tendo la zinaa Napiga goti nashukuru uwepo wa sanaa Kihisia nawapeleka kesho majamaa Majamaa walikua wavivu hawakukazana Waliishia kuamini kuwa kuna wingu la laana Waliseti mipango ila siku hazikufanana Huwezi kuikabili kesho kwa mbinu za jana