Alizaliwa mashariki alifahamika mahali pote Alikuwa malaika wa ndoto zetu wote Walimwita Mwanajua kwa maana alijua vyote Alitamalaki nuru ilitua mahali kote Na kila mahala alipita watu walimuheshimu Hakwenda shule ila aliheshimika ka' mwalimu Alikuwa mzuri kweli lakini shobo hana Hakuna aliyemgusa kwani alikuwa wa moto sana Urembo ulimuweka juu hakushuka anga zetu Alikuwa maarufu kushinda hata bwana Yesu Hata watoto walimpenda walifanya sherehe Tuliobalehe alipopita tulimwaga mbegu Ilipofika asubuhi tulimuwaza yeye kwanza Ilikuwa ni kama desturi kumfata Tulikuwa hatuli tukasaza Tuliwaonea wivu rafiki zake Mekuli na Veneranda Walikuja madogo wajanja na mapesa Wakauliza mama ukivaaje unapendeza Wakamuahidi ndizi, mawaridi na hariri Lakini jasiri rangi yake ya asili ilitesa Warembo wa dunia na vivazi vyao Waliwaza kumfikia na ilibaki njozi kwao Wazungu walikuja na pozi kibao Walimkaribia mwisho walibabuka Ngozi zao Mwanajua... amepotea kama hakuwepo Mwanajua... ameondoka kama hakuja Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo Kitakuwepo tu kwa muda Mwanajua... Mwanajua... Mwanajua... Tulijaribu kutumia chambo Apite anase ili tuweze kutupia mambo Mitego iliwekwa aje atumbukie hapo Tuliishia kumwona mbali na mwisho kuumia macho Haki ya nani, kuna walo'diri kumwita Mungu Walitukuza walisadiki na kuabudu Na sisi alitupa nguvu Tuweze kupambana kutafuta pesa ili tu tuweze kummudu Manyoka waliyavua magamba yao Wapendeze ili waje waweze kupata fao Walitanguliza vyeti na madaraka yao Waliisha kufa tukawazika na haraka zao Licha ya utofauti wake Alikuwa mkimya hakuna aliyeisikia sauti yake Wenye wivu walichoshwa na mizingu Maana alingáa sana kiasi alizificha nyota kama wingu Naziwaza features zote complete Nilitazama sikuona diva wa ku-compete Bila ina ala make-up za kisasa Aliwaka sana. mtoto Fulani konki Mwanajua... amepotea kama hakuwepo Mwanajua... ameondoka kama hakuja Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo Kitakuwepo tu kwa muda Mwanajua... Mwanajua... Mwanajua... Yeah! Iwapi barabara isiyo na kona? Simulizi isiyo na mwisho? Makala zimeandikwa tupo na nakala tunasoma Imeandikwa upasuka inapovuma sana ngoma Vile alikuwa amesukwa ni kwere Alipofika ilikuwa ka' umeshushwa umeme Kwa uzuri utadhani amejiumba mwenyewe Tulihisi hatashuka milele Tulikosea kwani... zile sifa hazivai tena Imefika jioni na yeye hang'ai tena Ndege hawaimbi nyimbo, misa zimefungwa Wamwaga mbegu wote tumebaki dilemma Najiuliza, alifichwa na ndugu kwenye kaya? Au alinenepa kutoka aliona haya? Hakujua, tulishindwa kutafakari chanzo Maana alizima na hakuwa wa moto kama mwanzo Anatukumbushwa kuwa tayari inapofika zama Hatamu yake imefika, zamu yake imekwisha Hajaacha hata alama ya damu yake Amekufa na utamu wake Yarabi nasikitika sana Namkumbuka sababu hakudanganyika Nuru yake pahala pote ilitawanyika Toka mzizima pwani kote alipagawisha Aliondoka na mwisho alionekana ziwa Tanganyika Dhahania zimeandikwa alichoka pengine Aliondoka ili wang'ae nyota wengine Itakufa damu, itakufa nyama Nenda mwanajua nenda tutakumbuka sana Mwanajua... amepotea kama hakuwepo Mwanajua... ameondoka kama hakuja Mwanajua anatukumbusha kuwa kilichopo Kitakuwepo tu kwa muda Mwanajua... Mwanajua... Mwanajua...