Ah! watakwambia mi' wa kishua 'cause I'm cute and Niko juu kama human kwenye food chain Vile I look good and I got this cool slang Na nina rap skills ka' Sean P wa Boot Camp Watasema kuhusu my intelligence my balances Watakuambia kuhusu my Teammates my Alliances Watakuambia kuwa nina fans mpaka Kansas Na nina-ball pia nina-draw pia ni Enthusiast wa Science Watakuambia kuwa nina fans mpaka Marabu Watakuambia kuwa my brain is all lava-full Watakuambia kuwa nina perfume Ninayopaka kuwa ina karafuu na ina-smell wonderful Hawatakuambia kuhusu aliyenikanya hadi nikome Aliyenizaa akanilea akani Akanipenda, akani Akanifanya msafi mnione Silabi, ah! zinaunda vitenzi kwa irabu Kutengeneza mashujaa wengi wa vitabu Tarihi zinatungwa toka enzi za mababu Mi' nimeona shujaa wa kweli ni ajabu Sidhani, kama inatosha kusema "thank you Ukinihitaji just whistle and 'Imma' rescue Ni bahati leo niko hai, simple nafurahi kukuona Ukiwa happy and I'm grateful Kama nina nyota nyumbani nahitaji nini? Nahitaji nini? Uko moyoni mahala ambapo nahifadhi PIN Naku-post 'Insta' kisha naku-hashtag QUEEN Wapo ambao walifuga kiburi Wakazipanda mbegu wakavuna sifuri Walichana misamba wakavunja misuli Sikutetereka maana ulinifunza vizuri Umenifunza jinsi ya kuishi na pia Umenipa hekima umenipa misingi na njia Kisha ukanipa bega kubwa la kukidhi dunia Linanipa faraja pindi n'napohisi kulia Nani mjinga azuie mbegu bora kuchipua? Labda kama shamba limezongwa na mabua Umenilea 'Soja' nimekua, umenifunza akiba Maana umasikini kidonda natambua Niko mbali natafuta miradi sawia Mvua inanyesha radi nasikia Bado nasimama Imara Asante kwa kunilea vyema mama, Umeipa zawadi dunia Asante kwa upendo wako asante kwa kunipatia hifadhi Asante kwa mabusu siwezi kuhesabia idadi Asante kwa picha kali naiandikia dibaji We' ni shujaa nitasimulia vizazi Happy Birthday Happy birthday Happy birthday Happy birthday Ukubwa wa upendo wako hauwezi wekwa mchanganuo Nimekulia mahala ambapo kuwa mwema si chaguo Umenipa busara sihitaji tena mafunuo Ikiwa nimepewa funguo, ya kuifungua dunia Nasikitika kauli yangu sio rasmi But I'm sure you've always meant for some' big Maybe that's how Angel got to be You're a proven God to me Wimbo huu ni upendo wangu kwako Marafiki wanafurahia uwepo wangu japo Wapo kadhaa wanaochukia uwezo wangu Hawatajua wala kuikisia kesho yangu We' ni kioo naona lesson nai-reflect vile Naona pande naona mbele najiuliza Mi' ni nani nikusahau nikudharau Wakati wazi umenipa sababu moja zaidi ya ku-respect women Siwezi lipa tone la kamasi ulilonifuta Siwezi tafuta chozi la samaki lililovuja Siwezi badili muda kisha ukawa thamani Nikaurudisha nawakusanya wenzangu nawafundisha Tumweshimu mama, wapi tunda pasipo mbegu? Imeandikwa iwapi rutuba pasipo nyevu Usipojua umuhimu wa msingi kwa kuta ndefu Ni sawa na kuzipanda mbigiri na kuja peku We' ni sauti ya uchochezi, hasa n'napolega We' ni lugha we' ni kurasa yangu pendwa We' ni kitabu kitamu siwezi weka kando nikishika We' ni ka' kiini kwenye Atom We' ni Oprah, Michelle, Shyrose Bhanji We' ni Winnie Mandela, Sophia(sonia) Ghandhi We' ni kama paka mwenye roho tisa We' Serena, we' ni Stosh Fellie, Go Tifa You're my Violet my Rose and my lily ah! You're my best friend, you're my wishing star You're my sweet dreams my wonder woman My Cat woman, you are my first love and that's vivid You love when I'm broke and when I get paid Before and after my payday You love me anyway, so I surrender my Ego And my Arrogance and I'm singing happy birthday Happy birthday oh Happy birthday Happy birthday Happy birthday