Najivunia kulala na mkeo Nimevumilia sana na leo Nimeamua kusema sijali ka' utanikaba koromeo Utanivunja na kuniacha kimeo Kamwe sijutii katu Sijutii katu Piga kelele jaza umati sihofii watu Nimekubuhu mpaka inafika hatua Nimefanya mtaa mzima wanajua Nasifikirii ni rafu Kwa mitindo zaidi ya saba Na maumbile nimejariwa si haba Nilimpa raha kote kwenye gari na valanda Kama mfungwa aliyekutana na kahaba Ona mrume ndago bila kiwewe Kila uliposafiri mi nilipiga misele Aliponiita niliitika kuzizima kelele Na nilipofika nilihakikisha anafika kilele Alinipeleka mbali kwa misemo motomoto Hadithi njoo utamu kolea Ukihisi naongeza chumvi kwa maneno ya uwongo Ona alama ya meno kwenye mgongo alafu ngojea Ni hakika alinikumbuka kila mida Na aliponihitaji niliibuka bila shida Alipopata swali aliniona mimi kwanza Akajiita Jenny nikajiita Tarzan believe that? Alifika alikaza na kamba Aliweka mizizi ya kukata na panga Alichizika utasema mwehu Moyoni aliacha alama ka Ronaldo alivyoacha alama bernabeu Nilikuwa siufahamu ugoni Ah Kama kufumaniwa ni dhambi na nitapata adhabu motoni Nitaenda na tabasamu usoni Labda wakati ni sasa nimerudi kuenzi nafasi Napenda uhakika silengi bahati Naomba ujue kuwa mkeo mkeo hakupendi kwa dhati Kumlazimisha ni kumuezi hayati Sasa kwanini usinipige na ulivyojifugia misuli Nivunje mbavu zangu labda utajisikia vizuri Fanya maamuzi sasa maana najitia kiburi Niue leo walimwengu watafukia kaburi Najisikia uchovu na mihayo napiga Uliza hizi nyayo na nyika Nimetoka mbali fanya maamuzi tuhitimishe kikao Maana hata mimi nina mishe kibao Mishe hata wewe unazo mishe unazobadili Fafanua eleza na uweke mifano isawiri Huo ubishi kujikweza weka kando ukatili Leo ndio mwisho vinavunja ndoa yako batili Andika talaka ili tuondoke Maana maamuzi ni yako au chukua panga unichome Haukuitendea haki kura yako Kuchagua ndoa wakati sio jambo kubwa kwako Utakapo chukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako Anajua kuwa mkoa wa mbali una watoto Anajua kuhusu vikao na safari za uongo Anajua kuhusu kondomu ulizobana kwenye nguo Na meseje za wasichana wa chuo. Ulimkuta mwema ukamteka kiakili Ukamshawishi mpaka akakupa shehena ya mwili Akakupa moyo akihisi utaweka nadhiri Ukajisahau na kumwonesha asili Ya kwamba wewe ni mchafu tu Kipi unalopoka lakini? Ubaya ulipokuwa ubaya unachokonda ni nini? Mmoja amatupa mwingine ameokata yamkini Aliyetupa ni wewe na aliyeokota ni mimi. ah!! Ilikuwa sababu ya msongo wa mawazo Ndio maana uliona wife sio wa moto kama mwanzo Aliteseka kiasi alihisi ndoa ni sumu Na nikachukua maamuzi magumu Dongo kwako Nilimwokoa na nikamvusha bahari Maana muugwana vitendo maneno hayataangusha jabali Siku mwili hautagusa sayari Utamkumbuka na pengine utajifunza kujali Mpunga umeyumba umeanza kujishuku mzee Umerudi nyumbani baada ya kushindwa kumudu starehe Haukuwepo Kwenye shida ilipofuzu tarehe Ulikimbia na nilikuepo mimi pekee Ngoja nikuudhi unajua mwanao ananiita daddy Nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi Nalipa ada, ada usizokumbuka kutoa Mwanao amefikia barehe na nimemfunza kunyoa Nimemfunza ushahiri nimefumfunza kufanya mahesabu Nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu Nimemfunza sheria zinazoongelewa bungeni Na nilienda kumtetea alipoonewa shuleni Unahoja yoyote defensively Maana haujui kama wanalala na kuamka safely Haujui kuhusu family dinner Woman' s day, birthday zao haujui hata anniversary Haujui maumivu aliyoyapata moyoni Haujui harufu ya chakula alichopasha jikoni Haujui kuhusu depression Maana mara mbili nimemkuta amejifunga kamba shingoni Nampenda yeye amenifanya nipate ishara Amenipa counselling amenifanya niache sigara Anajua chakula nipendacho timu niipendayo Kinywaji anajua even my favorite Colour Wenzio tunatafuta familia ili tujenge wewe yako ni lini? Mkeo amesaliti ndoa sababu yake ni upweke sababu yako ni nini? You know what they say... what goes around comes around man Yeah thus true... so i wonder why you changed you use to be a good man What happened to you? Nakiri mbele za watu nilishiriki hii dhambi Uvungu wa moyo wangu unasema usaliti ni haki Nyajua kisu chako uniue ila naomba uelewe Sijavunja ndoa yako umeivunja ndoa yako mwenyewe Aah