Yeah yeah... innocent mujwahuki.dizasta Yeah yoh skiza Nyumba ndogo, leo nna ajenda Naona umenogewa kula mpunga wa mwenza Unajitapa na mimi ndo nlokuweka Nashangaa sana nashindwa bomoa nilichojenga Japo nimekujenga bila msingi madhubuti Nikiwa kwako huwa nyumba kubwa sikumbuki Natumikia kifungo Umenifunga kwakuwa timu yako inajua kutumia viungo Nimejaribu kutamba bila wewe Tatizo nkizipata huwa nakufata mwenyewe Sio kwamba nyumba Kubwa hainiwezi kunifikisha Ukweli kwamba utundu wako umeuzidisha We sio mnyama lakini ninakufuga Ka unajua siwezi kukuacha bei shusha Maana hauvumi lakini umo Nyumba ndogo nzuri tatizo inajengwa nje ya mifumo Najiuliza nitakwacha lini aisee Mshahara wenyewe mdogo sa kwa nini tushee Kwakuwa unapika kile ninachonunua mimi Nyumba ndogo naomba unambie utakua lini? Ah yoh mtaani umeshakuwa habari Hautaki kuolewa hautaki kuijua mahali Tambua kuwa unaniletea jua kali Niliwahi kukuchunia mwezi nikanunua gari Nyumba ndogo nina watoto nina mke na nna madha Cha ajabu nikipata mtonyo tu nakuwaza Raha tunapata ila natoa changu Na unapokea bila ya huruma na ndoa yangu Unanivua koti unanipa maji Unanipa majina ya kifalme unanipa hadhi Unanipa masaji unanipa kazi Ambayo hata nyumba kubwa huwa hainipagi Kuta 4 sita kwa sita unajipinda Sikuzoei kila nikija mitindo mipya Mingine ya kitanga na kichina Nalia kama mtoto mpaka nashindwa kutaja jina Kama ni dawa hii limbwata digitali Nikiwa nawe huwa nawaza sifiki mbali Kwakuwa sihudumii nyumba kubwa inanyufa Ndo maana nyumba ndogo ni imara kuliko kubwa Yeah sipendi unavyoniita dia au laazizi Ungenipenda usingenibana hadi saa hizi Utabaki nyumba ndogo kuwa mke huna hadhi Nguo kwenye maji nkutofautishaje na mtekaji Sawa mi nawe wote dunga dunga We ni spy unajuaje madhaifu ya nyumba kubwa Unataka utawale una wazimu nadhani Kivipi uite nyumba kubwa simu ya mezani Nilijenga nyumba kubwa kwa wenge mwenzako Sasa kwa usitulie nawe ujenge ya kwako Kama wewe pia ni nyumba na unajengwa kiuhakika Jiulize kwanini unajengwa kwa kufichwa Nyumba ndogo huu ni walaka kwako Nimechoka kuwa chini ya mamlaka yako Sipendi nakataa kuwa wakala wako Natangaza mwisho wa utawala wa zama zako Nayakosa majukumu Kama baba,nyumba ndogo kuingia rahisi kutoka ngumu Nilikujenga nakwenda kukubomoa Kwa sasa nahitaji kuijenga ndoa Asanteh