(Mzee wa busara anawangaa) (Mzee wa busara noma toka anasoma) Oh ho ho, mmh mmh, mzee busara huyu Kutwa tunakesha kuweweseka (Huyu bwana mwanga mzee wa busara) Wa busara mzee wa ndumba, juju, mtu wa kuwanga wanga Zuga yake ni mganga wa jadi, mila na dawa za miti shamba Mtu wa ngenga domo mshelisheli na lapsha Aombe kwenu mboga na chumvi sukari viishe upoteze maisha Hataka kama maitaji yenu ya akiba hala hala jirani mchotee japo kibaba Ana paka wake huyo akilia, "Nyau", basi nyumba ya pili tunazika mtu na tunamsahau Wa busara kala hasara mtu wa njala Ni mpweke mkeke empty mweupe yuko maja-lala Kutwa kushinda kwenye bao tu Anabadili mikao tu! Mzee wa busara huyu huyu, huyu huyu Vitoto vikipotea mtaani vinatolewa chini ya mbuyu Hana kazi, hana kibarua anaishiishi vipi kama si' ugagu unamsumbua Zake ni chuma ulete Akinunua kitu lazi tandika kwenye kibanda cha chinga muuza fegi, pipi, machungwa Faida yote ya kwake Juma eeh! Mwambie mama haruna aingize ndani watoto mapema Mzee wa busara kakorofishana na wakina John Mgema Yani ni off-off mtaani mashaka tele Sijui kwa nini huyu mzee kawa na roho ya kuwakere (ah, Busara unatuudhi) Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Ni mzee ambae tunaishi nae kwenye nyumba za kupanga Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Na tena majirani wanahisi huyu bwana mwanga Mzee wa busara Malaria inaanza we inapungua, inaanza we inapungua Wa busara mtu wa swala, masaa ishirini na nne amkunja mswala Akitenda kosa ukimsema tu anaanza kuzusha msala Atanuna hapo atazira hapo, mjomba kazi unayo Sa' nimsisitize mwanga kashalimwa kisago! Tuone je tukimpa mvua atatukaanga? Kingwendu analalamika eti tumbo linamuuma Hata ule mchezo wake amepunguza kucheza Kingwe-Kingwe-Kingwendulile chakula cha mwanga usile Mtoto wa mtaa wa tatu amerogwa Rangi tatu (eh!) Mchana alikuwa mzima, maskini amegeuka chatu, "Ughh-aghh" Aya sasa nini ugomvi huo? Mtoto wake busara kila siku anakula kwetu Tukishaanza kula wakwanza kupakua nyama Ukimkataza mamaa, anaenda kusema Kivumbi sasa usiku Na huu ni mwaka wa sita mama analalamika mguu Tumehangaika kwa ma-doctor weh! Ikashindikana Tukahangaika kwa waganga weh! Ikashindikana Sasa sijui twende tukaseme kwa Fred Tibaigana Au tuendelee kukaa tumuuguze mama Hapana inauma uchungu Umroge mtoto aruke kisa ameangua makungu Majani kasema adhabu hakuna zaidi ya marungu Na tukiona tumeshinda tu, tunakuachia Mungu Lakini jana tu usiku tulichanjwa chale sita Tukaanza kujiuliza humu ndani nani kapita? Madirisha yalikuwa yamefungwa, Rashidi mlango kafunga Sasa amepita pitaje kwenye kuta kwenye nyufa? Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Ni mzee ambae tunaishi nae kwenye nyumba za kupanga Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Na tena majirani wanahisi huyu bwana mwanga Mzee wa busara (Mzee wa busara anawangaa) (Huyu bwana mwanga mzee wa busara) Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Ni mzee ambae tunaishi nae kwenye nyumba za kupanga Mzee wa busara Vishawisi vimemponza mpaka kafanya msala Mzee wa busara Na tena majirani wanahisi huyu bwana mwanga Mzee wa busara