Kishore Kumar Hits

Rose Muhando - Adui Wako şarkı sözleri

Sanatçı: Rose Muhando

albüm: Kwa Nini?


Adui yako huyo ni rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Usipigane na huyo rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Mtumishi wa Mungu Sarah
Walimsema sana kwa sababu ya tatizo lake
Lakini Sarah alimtazama Mungu
Ndiposa Mungu akampa mtoto Isaka
Hebu tazama mtumishi wa Mungu Ayubu
Ni majaribu mangapi aliyapata?
Ah, watu walimsema tena walimcheka sana
Lakini Ayubu alinyamaza kimya
Ndiposa Mungu akamponya Ayubu
Adui zake wote wakaona aibu
Adui yako ni adui wa Mungu
Mweleze yeye atashughulika naye
Adui yako huyo ni rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Usipigane na huyo rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Mungu wangu nimekutumaini wewe
Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda
Umesema katika maandiko matakatifu
Adui zangu watakuwa adui zako
Tena ukasema katika Luka sita
Ah, wapendeni hao adui zenu
Watendeeni mema, wote wanaowaudhi
Ah, wabarikieni wale wanaowalaani
Tena waombeeni wote wanawaonea
Akupigaye shavu moja mgeuzie na la pili
Baas, mbona watazama kibanzi ndani ya jicho la mwenzako?
Ah, na boriti ndani ya jicho lako huliangalii
Baas, mbona watazama kibanzi ndani ya jicho la mwenzako?
Na boriti ndani ya jicho lako huliangalii
Adui yako ni adui wa Mungu wee, aha
Mwachie yeye ashughulike naye
Adui yako huyo ni rafiki yako (rafiki yako)
Mwachie Yesu apigane naye
Usipigane na huyo rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Watumishi mmekuwa mkisemwa sana
Katika huduma mliyopewa na Mungu
Msikate tamaa songa mbele
Katika kuziokoa roho za watu
Ili watu wapone, ufalme wa Mungu wauone
Mwachieni Mungu ashughulike na adui zenu
Adui yako huyo ni rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Usipigane na huyo rafiki yako
Mwachie Yesu apigane naye
Lelelelele leleleleee

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar