Hakuna mkate ngumu mbele ya chai Akili ni nywele zangu nilipaka Dye More wananidai femi supa dupa Fly Game iko A,ex anaregret Y Z me na nakafunga,ka nilook me nadunga Mistari zimeshiba Sembe zimemada unga Flow kachumbari nawachanganya na Lugha Yani Femi Wali Bora misamiati me na tunga Zinacome through sana ki wallah bin wallah Blue ticks kibao ka si pesa au biashara Wanachuna me na gwara Me nichui we ni Swara Lale flani mjanja waku sakanya ma Guala Mandume wanagwaya na mafaya ni za Kike Roho zinadunda ka Chidinma na Kedike Fresh kama Tropical fresh Vs PK I am so sick fuck Hope kid DK Hakuna cha cooky im Queen Kaka Empire Femi adi ticha basi skiza I should mentor ya One girl super killer kuja na Your Entire Right left uppercut Mpaka muite Messiah Si hivyo ndo inafaa,ni hivyo ndo inafar Chozi damu jasho zote zimejaa kwa Kitambaa Tumetoka mbali cheki vile tumefika far Nayo nayo bado no time nilivunja saa We chora saba me nasaka 6 figures Mbogi ya mafans kwa mambleina mid finger Na wanabore si wananibore Shado mado na bado hawana mado na wanaringa Ati Nimelost basi stima zimerudi Femi Mbona hurogi Basi mchawi amerudi Number bado ni one, nobody is badder than Hata nkitupwa kwa den I will never be Dan Ah And You're now rocking with the best Wachana nao wajam bado me nacome Zest Na Bars ni high calibre ata mkidunga vest I'm in a class of my own so msitry kuniTest Si me ndio yule Ngori Femi First Body Femi kama Hollywood Femi never Nolly So kaki waka sana me nawacha scene Gory So if I was you singekua happy ningeworry Ligi ni flani premier wakisleki me na Tinga Kaa rada niko kazi me na Winda yeah Usibishane na simba kwa Jungle Shiko femi one nimerudi kaeni Kando