Maji ya moto Kitendawili tega nikutege Kitendawili tega, tega Tega nikutege mwiba Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba Sizonjeee Sizonjee aheee sizonjee Sizonjeee Kitendawili Sizonje aaheee sizonjee Kumbukumbu yako ikoje katika kukumbuka Nilikuita sizonje ili uingie ndani Kwasababu kila anaeingia lazima atoke nje Sizonje, Sizo Za Nje Sizonje ahee Sizonjee Hapa ndipo walipovishana majoho yasiyoonekana Walisoma hapa, walimaliza hapa Kila kitu kiliishia hapa Walipokuja kwetu walituambia Wale waliosoma na kumaliza Walimaliza kila kitu wakafa Kama haujui bahari ilipo tumia mto kwenda Kitendawili tega, tega Tega nikutege mwiba Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba Sizonjeee Sizonjee aheee sizonjee Sizonjeee Kitendawili Sizonje ahee Sizonjeee Sizonje Kiukweli watu wanalia Wapo wanaolia kwa machozi Na wapo wanaolia kimya kimya Wapo wanaolia na wanaoendelea kulia Japo vulio vinatofautiana Wapo wanaolia kwa kuhisi wamedanganywa Wapo wanaolia kupoteza ndugu zao Lakina wapo wanaolia kuona kuna Msiba kwao Lakini marehemu ndio muandaaji Wali mweupe kwa shekheee, msiweke nyama za mifupaaaa Watoto kaeni wanne wanneeee, waandaaji tutakula uwani tena mwishoo.! Shida zilipohamia shuleni, nikaona nikuwahi kidogo Sizonje. Mtoto anapoulizwa "Nani atalipa ada?", "baba!" "Yuko wapi??", "kafa!" Mwalimu wa fasihi anapotoa mfano wa maiti maiti zinazotembea Wale watoto wanalia tena Kwahiyo Sizoo Huku nje watu wote wanalia tofauti Lakini msiba ni mmoja Unaonaje, tuzike kwanza au tuhesabu idadi ya maiti zinazotembea? Kitendawili tega Tega nikutege mwiba Kuku anayetaga hachinji, akichinjwa msiba Sizonjeee Sizonjee aheee sizonjee Sizonjeee Kitendawili Sizonje aheee Sizonjeee Sizonje Naomba ikumbukwe kwamba, aliyemfundisha Chui kula watu ni binadamu. Na anayekunyoshea kidole Kuwanaye makini naye sio muda mrefu atakunasa kofi. (Sizonje) Kuku ana hatua tatu katika ukuaji wake Huachwa kwanza atage, ujue utagaji na wingi wa mayai yake Tunamsubili atotoe tuhesabu vifaranga na mayai viza Ndugu zangu, inawezekana kweli tumechoka maharage Lakini kama tunataka nyama tusubirini kwanja banda lijae. Kitendawili tega, tega Tega nikutege mwiba Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba Sizonjeee Sizonjee aheee sizonjee Sizonjeee Kitendawili Sizonje aheee sizonjee Sizonje