Kishore Kumar Hits

Christina Shusho - Bado Nakungoja şarkı sözleri

Sanatçı: Christina Shusho

albüm: Nipe Macho


Hapo mwanzo mungu aliziumba mbingu na nchi
Nayo nchi ilikuwa ukiwa na utupu
Ngiza lilikuwa juu ya vilini vya maji
Roho ya bwana ikatulia josho wa maji
Mungu akasema iwe nuru ikawa nuru
Mungu akaiona nuru ya kuwani njema
Mungu akaitenga nuru na ngiza
Mungu akaiita nuru mchana giza usiku
Mungu akasema na liwe anga, kati ya maji
Likatenge maji na maji, mungu akaliita lile anga mbinguni
Mungu akapaita pale pakavu nchi
Makusanyiko ya maji akayaita bahari
Nchi itoayo mbegu kwa jinsi yake
Mti uzaao matunda na mbegu zimo ndani yake
Mungu akanena kuwa ni vema
Mungu akasema na iwe mianga
Itenge kati ya mchana na usiku
Iwe ndiyo dalili majira, siku na miaka
Mungu akasema maji yajawe kwa wingi
Ndege waruke juu ya nchi
Mungu akaumba nyangumi wakubwa
Akisema zaeni mkaongezeke
Ndege wazidi katika nchi
Mungu akasema nchi na izae kiumbe kwa jinsi yake
Mungu akafanya mnyama wa mwitu na wa kufugwa
Mungu akasema na tumfanye mtu
Kwa mfano wetu na kwa sura yetu
Wakawatawale samaki wa baharini na ndege wa angani
Wanyama na nchi yote pia na kila kitambaacho
Kwa mfano wa mungu aliumba mwanaumme na mwanamke
Zamu yangu, nakungoja useme
Na
Mungu akaona kila alichofanya na atazama, ni njema
Bado nakungoja
Kila alichosema kikatokea akaona ni njema
Bado nakungoja
Nami nakungoja, baba nakungoja, useme na moyo
Bado nakungoja
Ukisema na moyo, natiwa nguvu, nasonga mbele kwa kazi yako
Bado nakungoja
Sema na kanisa, sema na watu wako baba
Bado nakungoja
Ukisema leo wagonjwa watapona, ukisema leo matasa watazaa
Bado nakungoja
Ukisema leo viziwi wasikia, ukisema leo vipofu wataona
Bado nakungoja
Ukisema leo viwete watembee, ukisema leo mabubu watasema
Bado nakungoja
Sema na nchi, sema na viongozi, sema na taifa
Bado nakungoja
Ukisema leo hakuna vita, ukisema leo hakuna magonvi
Bado nakungoja
Ee bwana kwako wanakuja wote, kila mmoja kwa shida yake
Bado nakungoja
Wawafanya maskini wawe navyo nao wajitegemee
Bado nakungoja
Nimetambua kwamba unayo mengi niyaombayo kwako ni machache
Bado nakungoja
Bado nakingoja unifute machozi, nakungoja unipe mwedo mpya
Bado nakungoja
Mimi nakungoja utimize ahadi, nakungoja bwana nakungoja
Bado nakungoja
Baba nakungoja ujibu maombi nakungoja bwana nakungoja
Bado nakungoja
Baba nakungoja uponye wagonjwa wetu nakungoja baba nakungoja
Bado nakungoja
Bwana nakungoja uwape matasa watoto, nakungoja
Bado nakungoja
Mungu, wewe husemi neno kwa kuwa lina ukweli, bali neno lako ni kweli

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar