Naona pendo Kubwa mno latoka kwa Mwokozi wangu Niteleka na maji mengi yatembeayo baharini Lanitolea tumaini Ya kwamba nitatiwa nguvu Na niwe mhodari Kwa pendo kubwa la Mwokozi Lanitolea tumaini Ya kwamba nitatiwa nguvu Na niwe mhodari tena Kwa pendo kubwa la Mwokozi Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele Na pendo hilo kubwa mno Huyaondoa majivuno Na kunifunza haki kweli Uongo wote niuvue Hunituliza moyo wangu Huruma nayo hunitia Na sote tuwe na umoja Katika pendo la Mwokozi Hunituliza moyo wangu Huruma nayo hunitia Na sote tuwe na umoja Katika pendo la Mwokozi Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako (moyo wako Baba) Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele Nijazwe pendo hilo kubwa Inibidiishe siku zote Rohoni niwe na jukumu Nimtumikie Bwana Yesu Hazina Yako nipeleke Kwa watu waliopotea Wafahamishwe pendo kubwa Ulilonalo Mungu wangu Hazina Yako nipeleke Kwa watu waliopotea Wafahamishwe pendo kubwa Ulilonalo Mungu wangu Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele Hallelujah Ni pendo kubwa Linalotoka moyo wako Ee Mungu wangu nakuomba Nijaze pendo lako tele