Mzee alisema hakuna cha bure Huo msemo tunautafsiri kinyume ee Hata shule kuingiza mtoto Lazima utoe mchoto Kupata simu ni balaa Road license bei nafuu 'tanunua Kupoteza ID ni mashaka, twarudisha jamhuri yetu nyuma Nchi ya kitu kidogo, ni nchi ya watu wadogo Ukitaka chai ewe ndugu, nenda Limuru(nenda Limuru) Hata nyumbani ukipatwa na majambazi, kupigana naye wasema sisis hatuna gari Lete elfu tano ya petroli, saidia utumishi Mahakamani hela ndio haki Kwa elfu chache mshtakiwa ndiye mshtaki, Utajiri huwa ushahidi Twarudisha jamhuri yetu nyuma Nchi ya kitu kidogo Ni nchi ya watu wadogo Ukitaka soda ewe inspekta, burudika na Fanta Nchi ya kitu kidogo Ni nchi ya watu wadogo Ukitaka chai ewe mama, nunua ketepa (Aha) Huko Kenyatta madawa zimeisha Masheet zauzwa marikiti mia kwa mia Wafanyikazi waenda miezi bila pesa Ni bahati ukitibiwa Mzigo wetu unazidi kuwa mzito Watoto wanne na mshahara wa elfu mbili Mia tano ya vitabu viatu na vyakula, nauliza na Mbotela vje huu ni uungwana' Nchi ya kitu kidogo Ni nchi ya watu wadogo Ukitaka chai ewe ndugu nenda limuru Nchi ya kitu kidogo Ni nchi ya watu wadogo Ukitaka chai ewe mama, nunua Ketepa(nunua Ketepa)