Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero Umewahi kuangalia huko chini (aye aye) Mtu maskini akiiba mkate Atavalishwa pingu miaka minne (aye aye) Lakini tajiri anayezorotesha Umaskini wa nchi nzima (mwajijua) Anachekacheka na hakimu Baadaye wapo wote pamoja mikahawani Dunia ina mambo Kweli ina mambo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Nyuma ya kila mlango Dunia ina mambo Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero Ni dini gani inayoendeleza chuki (mambo bado) Kwa ajili ya bidii ya bin adam Mimi sina kazi (mambo bado) Warumi wachukia wakristo wengine Wengine wachukia Waislamu (bure bilash) Waislamu wachukia Wayahudi Na nguvu zangu zote singeweza hayo yote Dunia ina mambo Kweli ina mambo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Vituko na vichekesho Dunia ina mambo Shetani akamwuliza Mtakatifu Petero Ni kulala mnalala au vipi (hallo hallo) Mnaruhusu viongozi wa nchi tajiri Kumiliki nchi masikini (hallo hallo) Kwa mfano wananchi wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni Waliporwa mali zao au siyo (au siyo) Basi mbona walionyanyaswa wasipande ndege Na kwenda ng'ambo ili kurudisha haki zao Dunia ina mambo Kweli ina mambo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Mbele ya kila wazo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Kweli ina mambo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Mbele ya kila wazo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Kweli ina mambo Dunia ina mambo Dunia ina mambo Vituko na vichekesho Dunia ina mambo