Kwa kweli ulinipenda nikiwa bado sijakujua Ukanipa mwanga wako nisije kwamba nikateleza Ukaniita mwana wako, vidonda vyote ukaviziba Na sasa niko huru, lawama yote ulijitwika Ni wewe tu, muumba vyote ulinipenda Ni wewe tu, maisha yangu kafanya mapya Ni wewe tu, tulizo wa moyo wangu Ni wewe, ni wewe ni wewe Nauliza, nimuishie nani mimi Nauliza, nimuabudu nani mimi Jehovah nimenyosha mikono, nitakuabudu milele Muweza, unaweza, na hakuna kama wewe Nauliza, nimkimbilie nani mimi? Nauliza, nimuogope nani mimi? Masiya, hakuna haya ya kukimbilia wewe Kwa maana nimeona hakuna kama wewe (Refrain) Hakuna, hakuna, mwenye penzi kama lako Baba Hakuna, hakuna, baraka kama zako wewe Hakuna, hakuna, aliyenifia ila wewe Hakuna, hakuna, ee ee (Refrain)