(Jam on the beats) Eh! Oya mitaa niliotoka police wanauza gongo Hata uwe mkweli huwezi ishi bila uongo Mlo mmoja na bado tulibeba nondo Na maisha yakasonga tu Eh! Ili sabuni zisiishe tulinyoa madongo Tulakala maharage hadi tukawa wachezaji wa ndondo Oh si' tumetokea Bongo na maisha ya nasonga tu, oh yeh Nishazika wanagu nilowapenda Ukija mtaani kwangu kutwa defender Kukimbizana January mpaka December Aah, eh-eh! Chumba kimoja wanalala dada na kaka Watu hawatupi msosi hata ukichacha Baba jambazi, mtoto anajiuza mataani Mama mchawi nyumbani atabaki nani? Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion Eh! Tumeishi na watu wanaoamini kwenye mpango wa Mungu kuna mkono wa mtu Tumeishi na watu wanaoamini sikukuu ndio siku ya kuchinja kuku, oya we (oya we) Tumeishi na watu wanaotembea na umeme lakini bado nyumbani walikosa luku (walikosa luku) Eh! Tukaishi na watu ambao wanaoamini kwamba bahati-Bahati zote alipangiwa Bukuku Hapo mwanzoni waliamini hatutopata mafanikio Waliotufagilia wakauza mafagio Eh! Mtaani kwetu sio Mtu aliotoboa sana alitoboa sikio Chumba kimoja wanalala dada na kaka Watu hawatupi msosi hata ukichacha Baba jambazi, mtoto anajiuza mataani Mama mchawi nyumbani atabaki nani? Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion (champion, champion) Wimbo unanikumbusha mbali kipindi naitwa Ima' Dharau, kejeli, manyanyaso ka' yatima Na ivyo ndo vimenikomaza mpaka leo nimesimama Ah! I thank God kwa hii power na heshima Ni'shatembea kwa miguu toka Manzese mpaka Temeke Kuomba nafasi ya kuimba na bado na iyo sipati Dharau zao na manyanyaso mli'fanya tamaa n'sikate (dah!) Pumzi inakata, koo linakauka Na bahati mbaya hata mdomoni sina mate! N'kapiga moyo konde n'kamuomba Mungu niongoze Na nikaweka nia kwamba mziki utanilisha Mziki utanivisha, mziki utanitajirisha Maisha ya zamani hayafanani na ya sasa Ni'sha sota sana acha tu nile bata Ma-deal mengi sikuizi, na sign angani Naitwa Raisi wa kitaa, napendwa mtaani Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion (champion, champion, champion) Ah-yeah, I'm the winner I'm the champion (champion, champion, championi) Mi' nachekaga tu Yeah! (Mafiaa)