DUNGA MAWE Jam on the beat Anaitwa dunga mawe Mwanangu wa utoto Katika kitu nakumbuka Alipitia changamoto Mwanangu dunga mawe Alikuwaga kibokoo Na sura yake ilitumika Kutishia watoto Eeee Oya huyo mwanangu alikuwa msela ALishawahi kufungwa akatoroka jela Maisha yake visanga yani mpelampela Asa ngoja niwape movie hilo lilikuwa twela Eeee Kuna kipindi dunga mawe si alipata mwali Tukaenda hadi ukweni si kutoa mahali Baada ya vitu kukamilika tulivyopewa mwali Akamvizia baba mkwe akamwibia mahali Alianza kuvata bangi na miaka saba Ulivyofika wa nane akaanza kukaba Sababu ya hali ngumu kakosa msaada Eee Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa Ndugu wa karibu hawakumpa faraja Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa Aaaah aah Anaitwa dunga mawe Aaah aaah Mwanangu dunga mawe Aaah aah Anaitwa dunga maawe Aaah aaah Mwanangu dunga mawe Ukimletea unyonge lazima aruke nawe Bora ukabwe na tonge ila sio dunga mawe Utafanya kitu gani hili umfanye apagawe Kashaoga matusi mpaka akaamua anawe Ile siku dunga mawe akiamka vizuri Tena ukamkuta kwenye mood Anaweza agiza bia mbili Afu akakupa mia mbili Kisha akasema kwamba chenji inarudii Demu wake dunga mawe alikuwa na mimba Yapata kama miez tisa Kwa kuwa pesa ya uzazi ilimshinda Ikabidi awe anapiganisha Akamwambia kwamba mpenzi wake kuwa amepata safari Anaenda kupambana hili mambo yawe shwari Na atakaporudi watakwenda hospitali Aaaahh Eeee Kumbe alipanga kwenda kuiba huko sehemu za mbali Ndipo akakamatwa na watu wenye asira kali Wakamshushia kipigo Kipigo juu ya kipigo Namwisho wakamchoma na mipira ya magari Aaaaa aaaah Anaitwa dunga mawe Aaaaa aaaah Mwanangu dunga mawe Aaaa aaaah Anaitwa dunga maawe Aaaa aaah Mwanangu dunga mawe Alianza kuvata bangi na miaka saba Ulivyofika wa nane akaanza kukaba Sababu ya hali ngumu kakosa msaada Eeeee Hakuwahi kuwa na mama wala huyo babaa Ndugu wa karibu hawakumpa faraja Mali alizoachiwa na wazazi waakee kadhurumiwaa Aaaaa aaaah Anaitwa dunga mawe Aaaaa aaaah Mwanangu dunga mawe Aaaa aaaah Anaitwa dunga maawe Aaaa aaah Mwanangu dunga mawe