I know you are image of me Mitaa inasubiri uhalisia Nami siwezi tabiri au kubashiri wapi ntaishia Waza fikiri na zingatia utandawazi umeshamiri Na bado unaathiri watanzania Dhima za fasihi ni elimu na burudani Sana ni msanii mc ndio me fanani Hadhira ananiskiza najibu anachokiuliza Nafanyiza miujiza naumiza na kupuliza Yoyote anaejiita mbishi naamini ananikubali Underground wanawish kwa kila hali na mali Wakifata nyayo zangu hakika watafika mbali Ninapofanya kazi zangu najali na kuwa mkali Naheshimu kila mtu tajiri na masikini Roho safi roho za kutu malaika mpaka majini