Kishore Kumar Hits

Marlaw - Rita şarkı sözleri

Sanatçı: Marlaw

albüm: Sungura Na Fisi


Ooh Rita, Rita
Ooh Rita, Rita
Ooh Rita, Rita
Ooh Rita oh no no no
Sauti inasikika tega makini
Hujui nani inamwita iih iih
Chozi latoka nitazamapo angani
Naona sura ya Rita iih hii
Ona mikono yangu mitupu
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo
Umepotea sikuoni kamwe
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
Aaah Rita we unajua jinsi gani mimi na wewe tulivyopendana
Jitoa sadaka kimapenzi ilimradi tusijetengana
Ila we unajua ni yako familia
Damu yangu ya Bongo si ya Asia
Ndo kigezo cha wao kunitosa mara mbili risasi wamenikosa
Kumbuka ile mimba ndio iliyokufanya
Ukaja kwangu (ulifukuzwa kwenu)
Ulijifunguapo mtoto na wote
Mkaishi kwangu (ukawachukiza kwenu)
Na taarifa ikaja kwako wewe Rita
Uende Arusha nduguzo wanakwita
Ukani-kiss kiss mimi na mtoto
Nikakukiss hey hey
Sauti inasikika tega makini
Hujui nani inamwita iih iih
Chozi latoka nitazamapo angani
Naona sura ya Rita iih hii
Ona mikono yangu mitupu (ona mikono yangu)
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo (hata nyumbani kwangu)
Umepotea sikuoni kwamwe (haupo)
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
Ni tangu Arusha hadi Iringa simu inaita napokea unalia
Kurudi Iringa uishi nami ndugu zako wamekuzuia
Ukasema laiti ungejua usingekubali uondokee pekee
Mwanao analia, ona mumeo ni bora ninywe pombe
Ila kwa penzi uka-force kurudi
Piga simu mume wangu nakuja
Na maneno ya konda kwenye basi ulifika
Alikupa siti ukakaa, ulipokaa ukakaa
Ile siku mi nimelewa
Niko mi na mwanangu kumpokea mke wangu
Konda akasema si wewe, ila tu mwili wako
Sauti inasikika tega makini
Hujui nani inamwita iih iih
Chozi latoka nitazamapo angani
Naona sura ya Rita iih hii
Ona mikono yangu mitupu (ona mikono yangu)
Imezoea kukushika we
Hata nyumbani kwangu haupo (hata nyumbani kwangu)
Umepotea sikuoni kamwe (haupo)
Ooh Rita, ooh Rita
Daily nakuwaza wee
Ooh Rita, ooh Rita
Mimi nitanyamazaje?
Ooh Rita Rita ahh na Marco Chali
Ndani ya MJ Records
This is true story to Marco
Rita, Rita, Rita
Aaah hata nyumbani kwangu haupo!!

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar