First time nilipenda nikajiona nimefika Nikajua sitotendwa machozi yasinge nitoka Nikajihadaa nikajawa na furaha Mwishowe kushituka nimezimia balaa Kaniacha ingawa alijua kabisa Pasi na penzi lake mimi sina maisha Akaniumiza nikadhoofika Nikajifariji na siku zikapita Nakumbuka nikasema sitokuja penda tena Baada ya miaka kupita nikajiona nishapona Nikayasahau maumivu ya nyuma Na nikajikuta nimependa tena Sikuamini kabisa kilichotokea tena Machozi ya mapenzi kunibubujika tena Ikanifanya nasema sitaki kuumizwa tena tena Wengine mbona wanajali upendo Wengine mbona mwaumiza tu Nyinyi nimewapatia langu pendo Wakalivunja na kuacha vidonda Wengine mbona wanajali upendo Wengine mbona waumiza tu Nyinyi nimewapatia langu pendo Wakalivunja na kuacha vidonda Kila ajaye hunitumia na kwenda zake Hathamini uhitaji wa moyo wangu kwake Nami nimekua kulia na kupona Kila siku bora kutopenda tena Najua ni vigumu kuishi bila penzi Lakini bora hivo kuliko machozi Sijui labda mi nina mkosi gani? Wengine mbona wafurahi penzini? Tamu ya mapenzi siijui mimi Chungu na mimi maumivu moyoni Tamu ya mapenzi siijui mimi eeh Tamu ya mapenzi siijui mimi Chungu na mimi maumivu moyoni hey (ooh) Wengine mbona wanajali upendo Wengine mbona mwaumiza tu Nyinyi nimewapatia langu pendo Wakalivunja na kuacha vidonda Wengine mbona wanajali upendo Wengine mbona mwaumiza tu Nyinyi nimewapatia langu pendo Wakalivunja na kuacha vidonda