Kishore Kumar Hits

Lady Jaydee - Siri Yangu şarkı sözleri

Sanatçı: Lady Jaydee

albüm: Binti


Nakuambia, aah siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza, aah siri yangu
Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu

Tega sikio kwa makini nikueleze
Hakuna tamu penzi kama la milele
Muda unaenda mwenzenu mi nagundua
Moyoni mwangu katu halitopungua
Nimeumizwa mara nyingi nakumbuka
Kuna hatua ilifika mi nikajuta
Lakini sasa 'na imani yupo wa kumpa
Ninachohitaji ni muda aweze tokea
Siwezi sema kuwa sitopenda tena
Kwani nitakuwa naidhulumu yangu nafsi
Moyoni najua ninalo penzi la milele
Na halitokwisha nakwambia labda wa kumpa asizaliwe
Nakuambia, aah siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza, aah siri yangu
Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu

Kuna aliyeniomba nimpatie pumziko
Kwa madai kuwa alichoshwa huko atokako
Niliyempenda nilimwambia nakupenda
Nililia machozi kwa yeyote aliyenitenda
Aliyenichosha nilimwambia waweza kwenda
Kuna aliyenifanya mapenzi yakanitatiza
Niliyemkosea niliona umuhimu wake
Nasisitiza kuwa 'na penzi la milele
Moyo wanituma wan'ambia kuwa na subira
Mimi nasema sitoimba tena nalia
Iliyobaki ni kusema nimekubali
Sitokaa tena kulia mimi na mawazo
Nakuambia, aah siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza, aah siri yangu
Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu

Unaweza toa pendo lako kwa furaha
Kumbe moyoni umejijazia karaha
Hutakiwi juta kwani katu hutojua
Unayempenda yeye atakuzingua
Mwisho wa yote ikawa ni matatizo
Yanayopelekea kuwa na mengi mawazo
Unachotakiwa, binti, usiusemee moyo
Kwani hutojua umpendaye naye akupenda hivyo hivyo
Niliwahi kumwimbia mpenzi wangu
"Sema unachotaka" ni wimbo uliofuatia
Lakini pendo hakuna bali ni kutendwa
Nimeamua kuwa komando Binti Machozi
Nakuambia, aah siri yangu
Kwa kuwa wewe ni wangu tena mshikaji siku nyingi
Nakueleza, aah siri yangu
Inayohusu maisha yangu inayosumbua moyo wangu

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

20

2021 · albüm

Benzer Sanatçılar