Mnh! Habari gani kaka naamini unanisikia Mi mzima wa afya mama mungu anasaidia Toka ulipotuacha mahututi anazidiwa Bibi presha presha nae akatangulia Bado twakuombea ulale salama pema Japo moyoni nna dukuduku Natamani kusema, niseme eeh Zile mali wosia ulizotuhusia Tuligawa salama Zuwena zote tukampatia Tusiwe ndugu lawama Ila... Zuwena kaka, amebadilika sana Yani shem lake bi Zuuh wa leo Sio yule wa jana Natamani ungemuona (Zuwena) Japo ungemuona (Zuwena) Kidogo tu ungemuona (Zuwena) Ungemuoona (Zuwena) Ooooh ungemuona (Zuwena) Ahh zuwena (Zuwena) Ooooh ungemuonaa (Zuwena) Zuwena oooooh ♪ Mmh Zuwena sasa kawa chotara Sio tena cheusi mangara Ngozi kaichubua awe Muzungu Anavuta na sigara Mara Boko, Mwananyamala Anachezesha tu miamala Kutwa anaisugua kipepe rungu Tena peku bila ndala Zuwena skuizi anabandika kope (Zuwena) Zuwena mipasuo kama yote (Zuwena) Oooh Zuwena, lipa shika tuondoke (Zuwena) Ahh Zuwena wanamuita chawote ooh ooh Juzi kabebwa kwa jirani ata hajitambui (Zuwena) Yani kalewa tafarani kautwika mbwii (Zuwena) Zuwena sio tena wa ibada na dini Sadaka chenji asaidie Skuizi kageuka pedeshee wa mjini Kutunza bendi wamsifie Na lile gari lako urithi wa babu La kulishia ng'ombe Skuizi kama kwato kwenye vilabu Linabebea pombe Mama tete kitandani hawezi ata kutembea Zuwena ameshindwa ata kuja kumuona Panadol kumletea Natamani ungemuona (Zuwena) Japo ungemuona (Zuwena) Kidogo tu ungemuona (Zuwena) Ungemuoona (Zuwena) Ooooh ungemuona (Zuwena) Ahh zuwena (Zuwena) Ooooh ungemuona (Zuwena) Zuwena oooooh ♪ Skuizi kataradadi anadanga Anakula ndizi kwa maganda Anajiita J Lo, Anadanga Anakula ndizi kwa maganda Eti Mzungu mweusi anadanga Anakula ndizi kwa maganda Na anatunyoosha Baba anadanga Anakula ndizi kwa maganda