Yeyeee baby. baby Yeaaahhh... Niliambiwa mapenzi upofu Katukatu nkawakatalia Kwako usikue na hofu Kabisa nikaweka macho ya bandia Kumbe na chunga mzinga wa nyuki Bila kuhofia kuumia Hadi kwa rafiki nikajenga chuki Ili kifua kukukingia Ukanipa tunda kinzani Bila kujua lina miba Kwa kusahau tena sidhani Nikaweka matanga bila msiba Nilijitahidii kuyaficha mengi wasione Macho shahidi Kinachonifanya nisonone Uliponilaghai ni mwanya Kumbe ni pengo na unajua Ikanifanya nikupende sana Mwishoni kichwa ukasumbua Kwa yote uliyonitenda (hongera) Uliniumiza mie Kwa vingi ulivyo vifanya (hongera) Acha ukweli nikwambie Kwa yote uliyonitenda (hongera) Uliniumiza mie Kwa vingi ulivyo vifanya (hongera) Acha ukweli nikwambie Ulidhoofisha kauli yangu Kwa kutumia ndimi zako Ikanilazimu nafsi yangu Kuchukia uwepo wako Nyingi ahadi ziliweka kutu Zakusubili ubadilike Kumbe cha mtu huliwa na mtu Ikanifanya nifadhahike Ulikata kwa nyembe Nyuzi nyembamba ya furaha yangu Ukanifanya nisipende Ule udhalili na utu wangu Nilijitahidii Kuyaficha mengi wasione Macho shahidi Kinachonifanya nisonone Uliponilaghai ni mwanya Kumbe ni pengo na unajua Ikanifanya nikupende sana Mwishoni kichwa ukasumbuaa Kwa yote uliyonitenda (hongera) Uliniumiza mie Kwa vingi ulivyo vifanya (hongera) Acha ukweli nikwambie Kwa yote uliyonitenda (hongera) Uliniumiza mie Kwa vingi ulivyo vifanya (hongera) Acha ukweli nikwambie Oooohohh... Kwa yote ulionitenda Uuuuuuh... hongera...