Pasha maji weka moto Tandika jamvi naja nyumbani Nimekuletea zawadi Kijora cha mkopo Futa la nazi ujipare honey Na vijisabuni vya magadi Nguru usimtoe chumvi ndio ladha yake Muunge tu nipe na chuzi na nyama yake Eeh kula ya mbuzi ni kamba yake Ye king'amuzi ni dishi lake Fungeni maturubai (Mkeshe mkisema) Wala hamtupi shida (Mkeshe mkisema) Ndo kwanza tunajidai (Mkeshe mkisema) Kama afisa wa nida ooh Tena daktari nimekuja na tiba sindano (Leta nichomeke) Chunga kibinda mwali napita kwenye mabano (Leta nichomeke) Nipo ngangari tayari kwa mapambano (Leta nichomeke) Chanya kagusa hasi leo mambo msuguano (Leta nichomeke) Tamba Tamba! Nakupa uwanja tamba Tamba Tamba! Warushe warushike roho zao Tamba Tamba! Wasokujua wakujuwe leo Tamba Tamba! Tamba mama nao ♪ Nitalinda benki kwa rungu niaminie Nikitaka langu mwana uvungu nainama mie Wavunje nazi na nyungu wajifushie Ooh moyo wangu atulinde mungu yasitufikie Nilishakumbwa na tsunami Na mapenzi nikalia nina amani kwako sasa Penzi si la unyang'anyi pekee yangu najilia Nashiba na kusaza Na ka TV kangu kanawaka kuzima (Nikupe) Na kasimu kangu japo ka mchina (Nikupe) Shika na moyo wangu nenda nao mazima (Nikupe) Tuzaliwa Mecca tufie Madina (Nikupe) Fungeni maturubai (Mkeshe mkisema) Wala hamtupi shida (Mkeshe mkisema) Ndo kwanza tunajidai (Mkeshe mkisema) Kama afisa wa nida ooh Tena daktari nimekuja na tiba sindano (Leta nichomeke) Chunga kibinda mwali napita kwenye mabano (Leta nichomeke) Nipo ngangari tayari kwa mapambano (Leta nichomeke) Chanya kagusa hasi leo mambo msuguano (Leta nichomeke) Tamba Tamba! Nakupa uwanja tamba Tamba Tamba! Warushe warushike roho zao Tamba Tamba! Wasokujua wakujuwe leo Tamba Tamba! Tamba mama nao ♪ Nishalinoa panga porini kukata muwa Mwana kaza kitanda usiku kuneng'emuwa Nishalinoa panga porini kukata muwa Mwana kaza kitanda usiku kuneng'emuwa ♪ Lalalala... lalalala