Yoh, yoh, yoh Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Congo Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo Hapana matata kitu roho inapenda mtapata Bongo Dar Es Salaama ni mpeto wa kutakata Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu Na pita Sleepway, Blue Pam au Mambo Club Kama hujazoea unaweza ukavunja shingo Mambo Isidingo watu mkononi Nokia bingo Huwezi kujua yupi mtoto wa geti, yupi changu Wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma Na toto mbili tatu za geti au za kona Hii watu wa Bongo tunasema napoteza mawazo Lakini mara nyingi hutokea wakati unazo Wakati wa dumba kali saa moja shuka utosini Na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni Na kama una gari watajazana madirishani wee Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani Kwenye madaladala kuibiwa ni kawaida Vaa cheni shingoni, saa mkononi utoe faida Wacha dirisha wazi kisha ukatize Manzese Ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese Rudi Mwananyamala oh! Mateja kibao Katiza saa moja moja uone roba za mbao Utaona kama mtoa roho yuko karibu yako Ni kheri utoe chochote ili uokoe nafsi yako Bongo eh Bongo Dares Salaam Utalia lia lia lia Bongo Dares Salaam Kaa chonjo eh Ndani ya Dares Salaam Utalia lia lia lia Ndani ya Dares Salaam Bongo ya sasa sio ya mwaka 47 Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba Sijui niseme nini ili muweze kunielewa Na sijui nifanye nini nisaidie wanaoonewa Hakuna heshima, ni vurugu mechi kwenye jamii Hakuna utii wala mafunzo ya manabii Na wezi wa mfukoni wanachomwa moto kinyama Mwingine hajaiba kapewa kesi kwa uhasama Nani atakae jua na sheria ipo mikononi?! Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao? Ni mshike mshike sometime ni vita na mapolisi Wao na sisi, rungu na pingu kama ibilisi Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku Na ni kama kuibiwa cheni kwenye ngoma za mchiriku Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi Masista duu wa Bongo wanazidi kupanda chati Huwezi kujua yupi wa Kigogo, yupi wa Masaki Mablaza majina yao ya asili hawayataki Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac! Ni burudani tosha, hivyo ni vijimambo tu Wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu Unaujua mstakabari wa ma-superstar wa Bongo? Lazma ufunzwe chuo kikuu cha mbwembwe za uongo City center, ofisi ni mtu aliposimama Hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli Akili kumkito ukilemaa umeachwa ferry Aliyeuziwa cheni katoa hela bandia Aliyepokea hela nae kauza cheni ya bandia Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo Na una-set mambo mengine yaende kwenye mtandao Bongo eh Bongo Dares Salaam Utalia lia lia lia Bongo Dares Salaam Kaa chonjo eh Ndani ya Dares Salaam Utalia lia lia lia Ndani ya Dares Salaam Katikati ya jiji hata usikiri dili haziji Na ukitaka ku-win Bongo cheza dili na wale magwiji Naona vijana wa Bongo wanapenda safari kafiri Hata mkoba wanategua kitendawili Safari bado ni ngumu jamani msiende kwa nguvu ya ndumba Ujinga sumu acha Mwenyezi awahukumu Changa uchange uende kiwanja unachotaka Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka Maskani Kimara, watu kila siku magoni Jonas Kiwia wasalimie Washington Ukiweza pita Texas mpe hi Chief Son Na mkumbushe uzushi wa Bongo Dar es Salaam Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa Na kwenye night club ni lundo la kaka poa Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa Upinzani wa jadi Bongo haupo Simba na Yanga Matonya na Makamba, na Sitte na wamachinga Na kali kuliko zote upinzani konda na denti Wanaposhika mashati tu denti anapoketi Hakuna mnyonge, wala anayekubali kushindwa Ngoma ngoroigwa na wote wanataka ubingwa Na watu wana magari mpaka ya milioni 200 Kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitendawili Wasioamini ni wale wenzangu na mimi Mlio na imani iliyopo juu mngoje chini Mtangoja milele, na mtakufa bila kelele Kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetele Ndani ya Bongo! Bongo eh Bongo Dares Salaam Utalia lia lia lia Bongo Dares Salaam Kaa chonjo eh Ndani ya Dares Salaam Utalia lia lia lia Ndani ya Dares Salaam Bongo eh Bongo Dares Salaam Utalia lia lia lia Bongo Dares Salaam Kaa chonjo eh Ndani ya Dares Salaam Utalia lia lia lia Ndani ya Dares Salaam