Kishore Kumar Hits

PROFESSOR JAY - Promota Anabeep şarkı sözleri

Sanatçı: PROFESSOR JAY

albüm: Mapinduzi Halisi


Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Mi' ndo S.A. the Bingo yaani nyangema promota
Nataka niwasaidie nyie wote mnaosota (uongo uwo!)
Nataka niwapeleke Kigoma kisha Botswana
Halafu mtachagua Chicago au Alabama
Kilometa zimekata hata kununua dola tano!
Tilipe kabla ya show na huo ndio wetu msimamo
Mnapanga na promota mkutane face to face
Kuamini huwezi ukimuona tu unampa kesi
Promota majalala ana suti chini ana ndala
Sekunde chache tu eti ananigongea sigara!
Muda unavyokwenda promota anasema hajala
Huu si ufala! Kivipi mi' nijitoe kafara (haiwezekani!)
Umekuja kufanya biashara, au umekuja kuleta masihara
Naona unadharau yaani umeshaniona sakara
Aliponiacha hoi promota anaomba nauli (mama yangu!)
Eti atanilipa siku show ikiwa nzuri! (Nyambafu!)
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Nitakulipa laki nane lakini mkataba sitaki (nyambafu!)
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Jamani mna fifty hapo nichukue fegi?
Mapromota wote hivi mnanisikia (mnanisikia)
Siyo mkisikia hii nyimbo mnajifanya mnasinzia
Tukianza kuimba mara ghafla mko busy
Hamna cha busy hapa naomba mtusikilize
Nawakilisha hiki kilio kwa niaba ya wasanii
Awe anaimba Rap, bendi hata kama R&B
Sasa kwa ufupi Mgosi na Jay tinasema hivii
Show zote maelewano hapo tisibishane
Kwanini kabla ya kupanda jukwaani tisimalizane? (Hela)
Kila mtu afe na chake eeh! Ndiyo maana yake
Msanii hamjamualika halafu mnatumia jina lake (aibu hiyo)
Matokeo yake tutaonekana si' tunaleta mapozi
Kinachofuata sasa hivi hapa ni kugawa dozi (kipigo)
Muziki ni kazi yangu msitake kunichezea
Unajifanya promota kumbe unatuongopea
Umeniita niimbe show zangu mimi ni za muhimu
Nakuja sababu mashabiki wetu si' tinawaheshimu (sana)
Nimeshuka jukwaani promota huwa hauonekani
Ni kutafuite kama Osama anavyotafutwa Afghanistan (alah!)
Kwa mtaji huu mi' nasema hapa hata haiwezekani
Kuanzia sasa mambo mapya siyo kama ya zamani
MC Kobogi unajua wanavyo tiambia (muongo)
Eti msihofu bwana n'tawanunulia bia!
Halafu huku kwetu mademu kibao wanawazimia
Nini kutuzimia? Wafe kabisa mi' sitaki hata kuwasikia (anasa)
Fanya unavyoweza hela yangu lazima kumpatia
Kama m'pombe, mnazi tinaunywa mpaka si tinaukimbia
Mapromota (nasema), mapromota
Jamani! Nitakulipa laki nane, lakini mkataba sitaki
Nitakulipa laki nane, lakini mkataba sitaki
Nyambafu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Nitakulipa laki nane lakini mkataba sitaki (nyambafu!)
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Jamani mna fifty hapo nichukue fegi?

Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Nitakulipa laki nane lakini mkataba sitaki (nyambafu!)
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Naamua kumpigia bila aibu anajisifu
Ngrii ngrii, eti promota anabeep!
Jamani mna fifty hapo nichukue fegi?

Поcмотреть все песни артиста

Sanatçının diğer albümleri

Benzer Sanatçılar