Kweli mimi nakiri yakwamba nimeathirika Mbio ziko ukingoni duniani nataabika Afya yangu inayumba nahara na kutapika Napiga goti natubu najua saa itafikia Baada tu ya kupima nikagundua sio mzima Na sasa ninajukumu la kuokoa jamii nzima Hakuna asiye tambua gonjwa hili ni la hatari Nilicho fanya ndugu zangu niliwapasha habari Wengi walinitazama kwa macho ya chini chini Eti kwa kuwa nnaupungufu wa kinga mwilini Na kila mwathirika wanasema amefanya ngono Na hii ndio sababu iliofanya nifungue mdomo Wengi wanasahau bado wanachangia sindano Viwembe na mikasi hospitali viwe mfano Watoto wameupata kupitia baba na mama Wazazi wanapokufa jamii inawasakama Na hii inatokea shuleni hata majumbani Poleni wote mnaotengwa na watu njiani Ipo siku itafika milango itafunguka Na maumivu makali ya dunia tutayavuka Msinitenge, ndugu zangu msinitenge Msinitenge, rafiki zangu msinitenge Na siku ikifika ikibidi mnizike Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechoka Msinitenge, ndugu zangu msinitenge Msinitenge, rafiki zangu msinitenge Na siku ikifika ikibidi mnizike Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechoka jamaa Nakwenda hospitali watu wananitazama Nashindwa kutembea manesi wananitukana Nguvu zinaniishia mwili wangu wote unanuka Ni nani wa kunishika japo anifunike shuka? Mwili wote unawasha sioni pa kujikuna Nawaomba msaada watu wote naona wananuna Nikune hata kwa mti japo unipinguzie uchungu Na mimi nitakuombea upate thawabu kwa Mungu Macho wamefunguka lakini mbele sioni Taswira ya jinamizi inatokea ndani ya mboni Watu wenye imani wananisalia kwenye kitanda Wenye roho nyepesi wameshaninunulia sanda Mafitini na wenye chuki kwa wingi waja kuniona Na dhani wanafarijika kwa hali wanayoiona N'nawataza usoni wengine wananicheka Kipi mnachocheka wakati mi' nnateseka Bora msingekuja mfanye party mburudike Waacheni wazazi wangu machozi yawabubujike Na kama mmenichoka ni heri mnimalizie Ili maumivu makali kesho yasijirudie Ila nawakumbusha yakwamba safari ni moja Nawaacha niwatangulie niendapo nitawangoja Hakika furaha yenu ya sasa itakuwa kilio Na kila mmoja wenu atazikwa kwa mapambio, mm Msinitenge, ndugu zangu msinitenge Msinitenge, rafiki zangu msinitenge Na siku ikifika ikibidi mnizike Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechoka Msinitenge, ndugu zangu msinitenge Msinitenge, rafiki zangu msinitenge Na siku ikifika ikibidi mnizike Kwenye makazi mapya nipelekeni nipumzike nimechoka jamaa Walimwengu nawauliza mbona mnaangalia pembeni Jamani mpo huru kama mnadukuduku semeni Nashangaa wengi wenu mnafurahi kuniona hivi Na eti! Kila mmoja anajiuliza mbona sifi? Najuta ila kamwe nasema sijutii kufa Najutia nafsi yangu adhabu itakayo ikuta Wengi mnadharau sana wagonjwa wa ukimwi Mnanicheka mimi mbona na nyinyi hampimi Ah, kama unajali nibora Angaza Okoa kizazi chako cha bongo kwa kujitangaza Ni nani aliyekwambia Condom inazuia ukimwi? Naona unajaribu kukausha bahari kwa ulimi Ukimwi hauzuiliki hata kwa Condom za bati Na dawa ni moja tu nasema acha uwasherati Wengi naona wanakuja tu, wapate cha kuongea Wengine mali zangu wameshaanza kuzigombea Ah, nikipata nafuu wengi mnachukia Babo najiuliza wangapi mtanifukia? Ni nani aliyewatuma hapa hosipitali mnifate? Maana nikiwashika mikono mnatema mate 'Uwezi kuambukizwa kwa kumshika muathirika Na pale unaponitenga najiona ndani ya gharika Ndio maana wasio na akili wanataka kuusambaza Wanatoa hela nyingi ni nani wauwakataza, kuwakataza