Naamka asubuhi niko chwiri tena mapema Nautoa mkeka sakafuni kisha naukunja vema Nawaza nitakula nini mentali kisha naguna Naanza kujikongoja kichwa chini mikono nyuma Naelekea kilingeni nilikopaki mkokoteni Nasaga na rumba kimshazali nyie acheni Nawapa hi machizi wananipa peace tunafurahi Tunapiga stori nyingi wallahi bila maslah Mara napata zali napeleka kago uswahili Wananipa buku mbili danga chee nazisunda chini Wakati natoka huku kijasho chembamba kikinitoka Nikaona toto ya nguvu nikajikuta nimeropoka "Dada habari samahani naomba niulize swali" Akajibu "Maskini koma tafadhali hii ngoma ya ghali" "Ehee unajua dada-" "We vipi hebu nipishe!" "Dada mbona mkali?" "Wee kinyago, kubali yaishe" Nikasema inshallah sawa hiyo yote kwa sababu ya fukara Nisije nikakubaka nitupwe selo nikawe kafara Nikaachana nae sehemu za nyuma akizitingisha Nilikula kwa macho hadhi yangu haikuridhisha Nageuza mkokoteni nakuelekea maskani Nikawapa stori machizi wakanicheka ikawa utani Siku moja nililemaa maskani sikuwa na tenda Na nilikuwa nikitafakari ni vipi siku itakwenda Kumbe kuna gari ilikuja na kupaki karibu yangu Sikuweza kuisikia labda sababu ya njaa yangu Nilishtushwa ghafla na mlio mkali wa honi Nilipatwa na mshtuko na hofu kubwa moyoni Kuangalia pembeni ilikuwa imepaki Toyota Surf Kulikuwa na sura ngeni ya malaika akaomba tafu Nilisita kunyanyuka kwa sababu nilikuwa mchafu Na alitoa elfu kumi na alikuwa akitaka dafu Nilipokea hela alichotaka nilimletea, akakipokea Tabasamu zito akanitolea nilimpa chenji "Ohh no keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend" Alikunywa maji ya dafu alitupa na kunikonyeza Niliganda kama nyamafu nikahisi alinibeza Alinipa busu la huba shavuni akanichombeza "I love you" akawasha gari akateleza Zali la mentali limetokea wakati mimi nnjaa Nikapendwa na demu mkali Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa Zilipita siku mbili nikiwaza kilichotokea Nikawaza yule ni mtu au jini amenitokea Potelea mbali uchawi hauendi kwa mentali Narudi nanyonya napuliza mentali nakuwa shwari Nabeba rumbesa nakatiza Samora Avenue Mara kwa ghafla mbele yangu inapaki Toyota Mark II Ohh napata ghadhabu mara nyingi sipendi dharau Naifuata gari kuanza kupaka mara nahema juu juu Aah ni yule mrembo! "Maskini pole sana mzigo mbona mzito kweli utafika nao salama" Natabasamu "Oh nimeshazoea mama Na namshukuru Mwenyezi Mungu kwani hii ni kama karama" Anakuwa mnyonge anang'ata kucha anantazama Anaaza kulia anatoa lesso anainama Namwambia, "bibie ni mara ya pili tunaonana Na sidhani kama ni mbaya iwapo tukifahamiana" "Naitwa Vicky na miaka 22 Ni mtoto wa kipekee kwenye familia ya kitajiri" "Oh naitwa Jay ukiniita fukara haukosei Na naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei" Alishuka toka garini na kusema "Jay nakupenda" Akaruka kwangu mdomoni na kuanza kupata denda Nilichomoka kwake na kuanza kurudi nyuma "Tafadhali mpenzi Jay jamani nionee huruma Acha kubeba mizigo panda ndani kwa ile mchuna Twende Mbezi Beach kwangu upepo unapovuma" "Sikiliza Vicky napenda tuwe marafiki Lakini hadhi yako hutakiwi kuwa na mtu wa dhiki Hata wazazi wako naaamini hawataafiki Tajiri na tajiri, maskini sithaminiki Tafuta kibopa mwenzio ili usishushe hadhi yako Mimi sistahili hata kuwa kijakazi wako" "Tafadhali Jay usitamke maneno hayo Naomba unielewe haya machache niyasemayo Hadi huu wakati mimi nimekupenda kwa dhati Ukikubali niwe wako nitajiita mwenye bahati" "Nimeelewa Vicky naomba niwahishe mzigo Tajiri ni mkorofi anansubiri Migomigo Na kila nikichelewa mwenzako napata kipigo Nasaga na rumba jua na mvua kwa mpigo" Tuliongea mengi akanipa hela za matumizi Sikuwahi hata kuziona nilikuwa kama chizi Niliacha kubeba mizigo penzi letu likaota mizizi Watu wa uswahili wakasema natumia kizizi Zali la mentali limetokea wakati mimi n'njaa Nikapendwa na demu mkali Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa Baada ya miezi mitano Vick alipata ujauzito Tulifurahi sana mambo yakawa mpwito mpwito Suala la kwenda kwa wazazi wake halikuwa zito Walifurahi sana kuniona tukafanya tambiko Walisema Jay maisha ya Vicky yapo chini yako Tumefurahi mmpendana kumlea ni jukumu lako Ilipangwa mikakati kamambe ya kufunga ndoa Watu hawakuamini ka mimi Vicky nitamuoa Ilifika siku ya siku mentali Jay ndani ya jumba Na Vicky ndani ya shela hakuna uchawi wala ndumba Tulishikana mikono ni nderemo na vifijo Tukafunga pingu za maisha kanisani bila ya fujo Furaha isiyo kifani lilifanyika bonge la party Watoto wa uswahili walibeba wali kwenye mashati (duh!) Zawadi zilizagaa, zilikuwa nyingi tena kemkem Baba mkwe alitupa Benz, kiwanda, nyumba na BM Acha zawadi nyingi kutoka kila sehemu Nilikumbuka nikacheka nilivyoteswa na wale mademu Mambo swadakta nipo na Vicky ndio my wife Kidume nang'aa wanajigonga shenzi type (shenzi type) Nilipokuwa arosto mlinikwepa kama ukoma Mambo juu ya mstari kunisalimu mnaona noma Sahivi napeta, nabadili gari full kipupwe Mlio nicheka wanataka ardhi ipasuke Naelekea kilingeni kuwapa dili machizi wangu Tena mara kwa mara siwezi kuwacha asili yangu Vicky ni Jay, Jay ni Vicky mustarehe Kutoka ndani ya dhiki sa kila siku sherehe Zali la mentali limetokea wakati mimi nnjaa Nikapendwa na demu mkali Na kuwaacha watu wote wakinishangaa, katika mitaa