Ooooh wowowow ooh Yeaah wooh Nimeamini Unataka uwe na mimi Watu wenye fitina Walileta majungu Uachane na mimi (yeah yeah yeah) Hivi kwanini Hutaki kuniamini Nyoyo ziko pamoja Mpaka siku ya kifo Uanze wewe au mimi (yeah yeah yeah) Wanachonga mama Wanaongea mengi hayana maana Mapenzi yetu ya kweli wanayapinga sana Wanafiki hawajui tulipotoka Hawataki kuona mapenzi yamenyooka Ona wanashangaa kuona penzi halichuji Ndio maana wanatunga uongo kwa makusudi Wengi walifurahi pindi tulipo gombana Weka maskio pamba ili tusiwape mwanya Nakuheshimu I love you honey Sogea karibu nami Basi panda kitandani (napata wazimu) Si utani bado unazo nishani kama zamani Wee pekee katika hii dunia Naomba tusahau mikasa tuliopitia Tulipanda milima mabonde na hali ngumu Ukanikumbatia ili mapenzi ya dumu Nimeamini Unataka uwe na mimi (mama) Watu wenye fitina Walileta majungu Uachane na mimi (yeah yeah yeah) Hivi kwanini (sema) Hutaki kuniamini Nyayo ziko pamoja Mpaka suku ya kifo Uanze wewe au mimi (yeah yeah yeah) Tumepita shida ngapi? Je walikuwa wapi? Ona wanavyo kuja Kwa kuona mambo safi Mbona wanakimbia pindi tuwapo na shida Wanakesha kuomba tuvishwe taji la miiba Kamwe huwa hawajengi wanataka kuharibu Kipenzi kuwa makini tuepuke majaribu Kila nikikosea nafsi yangu inanisuta Kweli kwako nakili siwezi kufurukuta Ni mapenzi yasio na mikuruzo Upendo na nidhamu ya kweli kwetu ni nguzo Wanataka tuharibu maisha ili wacheke Sitaki kukuona ukiwa mwenye upweke Nakuthamini jeeze Tuko pamoja jeede Tuongeze tu mapenzi ya dhati wajiulize Ni we pekee kwenye hii dunia Nakuaminia nakupenda pia (nakuheshimu) Nakufagilia wawa Nimeamini Unataka uwe na mimi Watu wenye fitina Walileta majungu Uachane na mimi (yeah yeah yeah) Hivi kwanini (sema) Hutaki kuniamini Nyayo ziko pamoja Mpaka siku ya kifo Uanze wewe au mimi (yeah yeah yeah) Wanajuwa kwangu hawataweza Na wanacheza Napenda unavyonijali Napenda kubembelezwa Namuomba manani daima uwe na mimi Nitakuwa nawe juu na chini hilo niamini Matatizo ndani ya luvo yapo tu hilo sipingi Kutafuta ufumbuzi hili ni suala la msingi Bora tuziepuke kesi za kutatanisha Tutulize akili ili tujenge maisha Hakika we umeumbwa wa udongo wa upendeleo Kuwa na wewe leo mi kwangu ni kichocheo Mi sina cha kusema zaidi ya nakupenda sana Hakika wewe ni wangu wa kufa na kuzikana Nimeamini (wakufa) Unataka uwe na mimi (nakuzikana) Watu wenye fitina Walileta majungu Uachane na mimi (yeah yeah yeah) Hivi kwanini (sema) Hutaki kuniamini Nyayo ziko pamoja Mpaka siku ya kifo Uanze wewe au mimi (yeah yeah yeah) Yeah Pro Geez Commando Jeed, Bongo record's Oooh wowowow