Umesahau ulipotoka hujui unapokwenda Ukapata kiburi kuona mi nakupenda Nilikuthamini na letu penzi kulienzi Na leo siamini kama umenisaliti mpenzi Kumbuka nilikukuta kijijini sigimbi Umebeba mahindi na furushi la magimbi Nguvu ziliniishia mithili ya kufa maji Nafsi nayo ikakidi kwamba mimi nakuhitaji Kigoli mwenye umbo kama la mdori Wala sikutaraji ungepiga nami stori Nilifurahi kuweza kukufahamu Na nikakuahidi subiri zangu salamu Kwa kuwa nilikwenda tu kumtembelea bibi Yote yaliyojiri tu kumweleza ilibidi Wote walishangaa kusikia namtaka mchumba Kwani vijana wengi wa mjini tuna kasumba Wakaweka kikao ndiposa niweze kutoa posa Niliapa kujua iwapo ningekukosa Walinikabidhi nirudi nawe mjini Na nikakusisitiza mjini kuwa makini Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandama Kuwa nawe haitawezekana mpenzi Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulana Alikuwa mzuri mithiri ya malaika Alipotua mjini Zubeda ni patashika Hakika alionekana alikuwa mgeni wa jiji NIlipovua viatu nilivikuta ndani ya friji Alifanya vibwenga washikaji wakanicheka Hakutaka kitanda alilala kwenye mkeka Alipokuwa akiona magari alikimbia Akimuona mtu kwenye TV anamuamkia Kila alichofanya alikuwa anakosea Nilimvumilia kwa kuwa hajazoea Hakai kwenye sofa alikuwa anakaa chini Mafuta ya kupikia eti anayapaka mwilini Namnunulia soda hataki anataka togwa Nikimletea keki hataki anataka boga Majirani walimpenda sababu ya uzuri wake Nasikitika mashangingi wakawa rafiki zake Akaanza kunywa pombe alipokwenda kusuka Usiku anatoroka tena kwa kuruka ukuta Nilipokuwa natoka, nae nyuma antoka Nikimtuma kitu anadai eti amechoka Nikienda kazini ndani analeta mabwana Magari ya kifahari yakawa yanapishana Hakika starehe za dunia zikamtenda Na hatimaye hata nyumbani pia akatoweka Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandama Kuwa nawe haitawezekana mpenzi Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulana Nilipigwa na butwaa, mtaani walinishangaa Nilikosa raha hata nafsi ilikata tamaa Sikujua huyu binti ni mzima au amekufa Ilibidi niombe watu msaada wa kumtafuta Kumbe anaonekana viwanja vya kila aina Leo yuko na mzungu na kesho yupo na mchina Nilipata shahuku ya kutaka japo kumuona Ingiwa niliamini moyoni ingenichoma Kweli tulimtafuta kwenye kumbi tofauti Ili nihakikishe kweli hajapatwa na mauti Nikamkuta casino la wadachi na walatino Akigonga mvinyo, wa hashipapi, hashipinyo Pechiechipinyo na pamba za mandarino Macho yalinitoka mithiri ya zingonginyo Hakika alipendeza kwa staili alizocheza Na kila aliyemtazama alitamani kumchombeza Kwa pozi na dharau alijifanya amenisahau Akaniona takataka mbele ya washikadau Ilibidi niondoke machozi yakinilenga Shetani kashanitega na tunda langu kamega Akapata mimba aliyempa hakumtambua Na wote aliowafata eti wakakana kumjua Zubeda na mimba yake hakuwa na pakuishi Hakujua ale nini na vipi apate ridhiki Ghafla hifadhi yake ikawa ni stendi ya basi Siku nyingine mvua ilimnyeshea kupita kiasi Akarudi nyumbani eti arudiane nami Kurudi kwao hataki, mi na familia ndani Nafsi yangu nilikupa uitunze mpenzi Anasa za jiji zikakuchanganya Mapenzi ukasaliti na ukanikana Ukaniacha dunia ikiniandama Kuwa nawe haitawezekana mpenzi Nshampata ambae tunapendana Majeraha makubwa yajadui moyoni Mi nimeshamuachia maulana