Uuunhuuhhh Joseeeph.! Ooohhhh.(Rama D - Introlude)
Eyo jifunze ya kwamba maisha ni vita
Dunia imekwisha, kila kiumbe anataka kupita
Najiuliza Je! ni siku za mwisho zenye miujiza,
Au ni maandiko ya vitabu tunayatimiza
Dini wana idhihaki, kuabudu hawataki
Mbio za utajiri kati yetu nani abaki,
Makaburi yanaongezeka pembeni maiti inacheka,
Hukumu inasogea ulimwengu unatetemeka,
Wanachimba chini wapande mbegu za fitna,
Chui kavishwa ngozi ya kima apewe heshima,
Watu wafe vibudu matendo yao yafuate,
Wanageuza ukweli kinyesi kuwa mkate,
Ni busara za nyoka na upole wa njiwa,
Wamelaaniwa na kusahau watafukiwa,
Dunia inaelemewa na mzigo mzito wa dhambi,
Karibu itaanguka, Muumba atavunja kambi,
Wanalea mimba ili wazae majungu
Yaani ni kichekesho, kuona mna-beep Mungu,
Huwezi kupinga jema na ukweli wenye utakaso,
Watalia machozi ya damu, na meno kutoa jasho
Jifunze, Ona, Sema, Elimika, Pitia, Hamasika
Hiii naamanisha Joseph x 2
Joseph Joseph
Ona shetani ameshika msaafu na bibilia,
Pambio anawaimbia, machozi anawalilia,
Maneno yanawaingia, mnaanza kumsifia,
Mwisho mnapigia goti na kuanza kumusjudia,
Sisemi mmekosea, aaahnh! hamjapotea,
Labda hamjafamu ni nini kitatokea,
Mnakubali mpewe ukimwi, eti! watawatibu,
Zinduka vua utumwa wa akili upate jibu,
Joseph maandiko ya kweli ndani ya vitabu,
Joseph ni mwongozo uletao wingi wa thawabu,
Joseph wanauliza maswali mi ndio jawabu,
Kukuheshimu na kuheshimu ila kujuana isiwe tabu,
Nasema tena na tena na tena kwa nia njema,
Kuuliza si ujinga na kujua si kilema
Hata Allah aliumba ulimwengu kwa lake neno,
Wote wanaolipinga kilio na kusaga meno,
Roho zetu akiba kwa jailli ya kuchomwa moto,
Paramia watoto, utajiri bado ni ndoto,
Bado naishi kwa pasi ndefu, niite Joseph
Na Muumba ananibariki kwa kusamehe wakosefu,
Jifunze, Ona, Sema, Elimika, Pitia, Hamasika
Hiii naamanisha Joseph x 2
Joseph Joseph
Elimika utahitajika na nafsi itawabijika,
Lazima uwe na jibu mbele ya hukumu ya malaika
Kilemba ulichojivika ipo siku kitachanika,
Utaabika zaidi ya mwenye ugonjwa usiotibika,
Pitia
Vitabu vyote bibilia na misaafu
Sikia
Sala zako ndizo zitaokoa wafu,
Na pia
Utahukumiwa kwa matendo yako machafu,
Dunia
Inaangamizwa na wale wenye Sarafu,
Hamasika mwisho wa dunia umeshafika,
Karibu yatatimizwa yale yote yaliyoandikwa,
Na haya nayo nena yatafika kila mahali,
Kama mfano wa Mussa alivyo-tawanya bahari,
J.o - S.e - P.h
Mi nikama sedoo kwa mc sihitaji ucheshi,
Sauti ya gheto si tu... Vina vyenye maana nyepesi
Hili neno turudi kwake lord of mercy,
Jifunze, Ona, Sema, Elimika, Pitia, Hamasika
Hiii naamanisha Joseph x 2
Joseph Joseph
Yeah.
Ni neno
Kutoka Tanzania, paka Africa nzima na Dunia,
Professor Jay, Choka Mbaya Baby,
Yeah
Bongo records
Yeah Yeah Yeah
Annh
Yeah
Поcмотреть все песни артиста